Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizindua baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mei 6,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson(Kushoto) akimkabidhi Kanuni za kudumu za kusimamia utendaji katika mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mtendaji wa mamlaka hiyo Godwin Everygist (kulia) Mei 6,2025 kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka hiyo katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri hiyo .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Willium Jijimya akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mei 6,2025
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoani Shinyanga Mhandisi.Eugine Soka akizungumza Mei 6,2025 kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mei 6,2025
Mwenyekiti wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Fabian Makongo akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo Mei 6,2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri Emmanuel Johnson kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo atakayedumu kwa miaka mitano.
Kaimu Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Omary Mwenda akizungumza Mei 6,2025 kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu.
Mtendaji wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu mkoani Shinyanga Godwin Everygist akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza hilo Mei 6,2025 katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Dionis Makala akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo Mei 6,2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri Emmanuel Johnson kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo atakayedumu kwa mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Willium Jijimya Kushoto(suti ya blue) akimkabidhi Kanuni za kudumu za kusimamia utendaji katika mamlaka hiyo mwenyekiti wa mamlaka hiyo Mhe.Fabiani Makongo kulia (suti nyeusi) Mei 6,2025 kwenye uzinduzi wa baraza la mamlaka hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mwananchi wa mamlaka ya mji mdogo Kishapu mkoani Shinyanga Anseli Mchale akizungumzia faida za mamlaka ya mji mdogo na uundwaji wa baraza lake lililozinduliwa Mei 6,2025 kuleta mabadiliko na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Wilaya yote huku wakitarajia huduma za kiserikali kuendelea kuboresha na sekta mbalimbali.
Na Sumai Salum-Kishapu
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Emmanuel Johnson amezindua rasmi Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu Mei 6,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Johnson amesema Kishapu ilitangazwa kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo mwaka 2004 haikuwahi kufanya kazi sababu ya changamoto za kiuchumi.
"Mbali na changamoto hiyo lakini bado wanaKishapu wamekuwa wastahimilivu na uelewa wa kukubari kupunguza vitongoji, kama tulivyosema Mamalaka haikuweza kujiendesha kwa sababu ya ukubwa wa vitongoji uliokuwepo tokea 56 hadi 11 ambapo viinapelekea kuwa na jumla ya wajumbe 17 wa Baraza hili",amesema Johnson.
Amesema serikali itasimamia na kuhakikisha Baraza hilo linafanya kazi zake kwa lengo la kuhakikisha wanafikia Halmashauri ya Mji wa Kishapu.
"Nichukue nafasi hii kumshukuru sana aliyekuwa Mkuu wa Wilaya yetu Mhe. Joseph Mkude na Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson uwepo wa Mamlaka hii kwa kiasi kikubwa inatokana na jitihada, juhudi na ushawishi wao",ameongeza Johnson.
Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita kuwa serikali ya yaliyoshindikana awamu zingine yamewezekana huku akitoa rai kwa viongozi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya wananchi wakishirikiana wao wenyewe pamoja na watalamu wa Halmashauri hiyo ili wafikie wanayoyategemea.
Amesema lengo la serikali ni kushusha madaraka kwa Wananchi ili wapate huduma karibu na maeneo wanayoishi hivyo watalamu pia wanapaswa kuwa tayari kutoa ushirikiano wakati wote.
"Kwenu wakuu wa kisekta tunahitaji kuona mipango ya maendeleo inaendana na hadhi ya Mji, katika Kata hizi za Mwataga na Kishapu hatuna kijiji tunategemea tukienda kule Lubaga tukute kuna umeme,maji na miundombinu mizuri ya barabara hivyo eneo lote la Mji Mdogo linapaswa kuangaliwa kama tulivyokuwa tukiiangalia Mhunze ikiwa makao makuu ya Halmashauri yetu", amesema.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Eugine Soka amewapongeza viongozi wote waliosimamia mchakato wa uanzishwaji Mamlaka ya Mji Mdogo na kufikia hatua ya kuwa Baraza kamili.
"Baraza hili linaundwa na wazawa wa Mji huu ambao ndio wenye wivu mkubwa wa maendeleo tunatumaini Kuwa mtaenda kutumia uzalendo wenu na ufanisi mtakao kuwa nao ndio utakaopelekea kupata Mamlaka ya Mji kamili kwa haraka kadiri ya jitihada zenu", amesema Soka.
Kaimu katibu Tawala wa Wilaya hiyo Omary Mwenda amesema viongozi waliochaguliwa wanapaswa kuwa wawajibikaji huku akiwakumbusha kusimamia ukusanyaji mapato, kuwahudumia wananchi na kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Willium Jijimya amesema Kishapu imeingia kwenye historia kuongeza nguvu ya kuchochea maendeleo kuongezeka kwa haraka.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani humo Shija Ntelezu amelipongeza baraza la madiwani na Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa mapato na kuwa mbunifu kupunguza vijiji na sasa wamefikia mahali wanapoiona ramani ya mabadiliko na maendeleo ya Kishapu.
Mtendaji wa Mamlaka hiyo Godwin Everygist amesema wamejipanga kuhakikisha Mji unakua katika miundombinu na mapato kwa kushirikiana na watalamu.
"Tunataka kuwa na Mji uliopangiliwa vizuri kimajengo,usafi wa mazingira tuwe na dampo lakini tutahakiisha tunazuia ujenzi holela na watu wafuate taratibu za ujenzi na kiutawala tuwe vizuri ili hapo baadae tufikie vigezo vya kuwa Halamsahauri ya mji kamili" amesema Everygist.
Mkazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu Anseli Mchale amesema kufuatia uwepo wa Mamlaka hiyo wanatarajia kusogezewa huduma mbalimbali za kiserikali na zipo fursa za kibiashara wananchi watazipata kwani mji utapanuka huku wakishuhudia uboreshwaji na upatikanaji bora wa huduma muhimu ikiwemo afya,elimu,barabara, maji na umeme.
"Tunashuhudia kuna taasisi hatukuwa nazo na sasa zimekiwepo mfano huduma za mikopo wajasiriamali wanaongezeka na kufanya shughuli zao kwa uhuru na amani kwani wanapata huduma kwa ukaribu", ameongeza.
Amesema watendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu wanalo jukumu la kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita kwa kujituma kwani Wananchi wanahitaji kuwaona wakifika kwenye maeneo yao kuwahudumia kwa kutatua kero zao ikiwemo usafi wa mazingira,migogoro ya ardhi pamoja upungufu wa huduma na baadhi ya vifaa tiba na madawa kwenye sekta ya afya.
Kabla ya uzinduzi huo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Bw.Omary Mwenda amesimamia uchaguzi wa viongozi wa Baraza hilo ambapo Mwenyekiti ni Mhe. Fabian Makongo na Makamu wake Mhe.Dioniz Makala na kuwa na jumla ya kamati tatu ikiwemo Uchumi,ujenzi na mipango,Elimu afya na maji pamoja na Uchumi ujenzi na mipango miji.