TUME HURU YA UCHAGUZI HAIKUJIANDA, POLISI WACHUNGUZE MATUKIO YA UTEKAJI-"CHADEMA"
Imeelezwa
kuwa tume ya Taifa ya uchaguzi
haikufanya jitihada za ziada kwa ajili ya kuhamasisha wananchi ili kujitokeza
kwa wingi katika kuhakiki kujiandikisha na kufanya maboresho katika daftari la kudumu la mpiga
kura hali iliyopelekea mwamko mdogo wa wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.
Hayo
yameelezwa Agosti 29,2024 na katibu wa chama cha
demokrasia na maendeleo chadema kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami katika
mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake ambapo
ameiomba tume hiyo kuongeza zaidi muda
wa uandikishaji na uhakiki wa daftari hilo ili wananchi wengi zaidi wapate
fursa za kuingiza taarifa zao katika daftari hilo na hatimaye waweze kushiriki
uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
“Tulibaini
hali ya mwamko mdogo wa watu kujitokeza katika zoezi hilo katika siku ya
tarehe 27 mwezi Agosti mwaka huu ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho ambapo
changamoto hiyo imesababishwa na tume huru ya uchaguzi kutokuchukua hatua za
ziada katika kuwahamasisha wananchi juu ushiriki wa zoezi hilo”amesema Mnyawami
Katika hatua
nyingine, Mnyamwami pia amezitaka mamlaka
zinazohusika na usalama wa raia kufanya uchunguzi wa kina kuhuisian na masuala
ya upotevu na utekaji wa wananchi unaoendelea katika baadhi ya maeneo hapa
nchini ikiwemo mkoa wa Simiyu ili kubaini kwa kina nani wanahusika na matukio
hayo na kuwachukulia hatua za kisheria
“Tunatoa
wito kwa jeshi la polisi mkoani
Simiyu kufanya uchunguzi wa kina juu ya matukio ya watu kutekwa na kupotea ili
kubaini chanzo cha tatizo ni nini hali inayopelekea wananchi kuwa na taharuki
na kuishi kwa hofu “ameongeza Mnyawami.
Chadema
kanda ya Serengeti ni moja wa wapo ya kanda maalumu iliyoundwa na chama hicho
ikiwa ni utekelezaji wa sera ya chama hicho ya kuweka mifumo ya utawala kwa
majimbo ili kurahisisha shughuli za utawala ambapo kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Shinyanga Simiyu na Mara
0 Comments