Header Ads Widget

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO NA MANISPAA YA SHINYANGA,WAMEPANDA MITI KUADHIMISHA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA MADARAKANI,KATIKA SEKTA YA AFYA

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO NA MANISPAA YA SHINYANGA,WAMEPANDA MITI KUADHIMISHA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA MADARAKANI,KATIKA SEKTA YA AFYA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
CHUO cha Sayansi za Afya Kolandoto pamoja na Manispaa ya Shinyanga,wamepanda Miti kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira, ikiwa ni Sehemu ya kuadhimisha miaka mitatu ya Rais Samia Madarakani,katika Sekta ya Afya.

Zoezi hilo la upandaji Miti limefanyika leo April 11,2024 katika maeneo ya Chuo hicho likiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Kolandoto Paschal Shiluka, pamoja na Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga.
Shiluka akizungumza kwenye zoezi hilo la Upandaji Miti,amesema anampongeza Rais Samia kwa Utawala wake uliotukuka ndani ya miaka Mitatu,kwamba katika Sekta ya Afya ameitendea haki na kuleta mabadiliko makubwa.

Amesema katika Sekta hiyo ya Afya, Rais Samia ameboresha huduma za Afya kwa kujenga Zahanati,Vituo vya Afya, Hospitali pamoja na kupelekwa vifaa tiba vya kisasa kwa lengo la kuimarisha Afya za wananchi.
Aidha,amesema Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika katika kuadhimisha miaka Mitatu ya Rais Samia Madarakani,wameamua kupanda Miti katika maeneo ya Chuo hicho ili kuenzi kampeni yake ya utunzaji wa Mazingira.

"Awali Chuo chetu cha Kolandoto hatukuwa na maeneo makubwa kwa ajili ya kupanda Miti,lakini sasa hivi tumeshapata maeneo baada ya Migogoro kumalizika na tumeanza kupanda Miti,na malengo yetu hadi kufikia mwakani tuwe tumepanda Miti zaidi ya 5000,"amesema Shiluka.
Msimamizi wa Mazingira katika Chuo Cha Sayansi za Afya Kolandoto Josephine Charles,amesema leo wamepanda Miti 150, na kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu kwa kupanda Miti ya kivuli,matunda na mapambo ili kufanya Kolandoto kuwa ya Kijani.

Waziri wa Elimu Chuoni hapo Rosemary Revocatus,amesema Upandaji wa Miti huo mbali na kupendezesha Chuo na kuyatunza Mazingira, pia watapata kivuli kwa ajili ya kujisomea na kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Naye Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga,amekipongeza Chuo hicho kwa kupanda Miti,na kwamba kwa kufanya hivi watahamasisha Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kupanda Miti ili kutunza Mazingira.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA 👇👇
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Paschal Shiluka akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji Miti.
Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji Miti.
Msimamizi wa Mazingira Chuo Cha Sayansi za Afya Kolandoto Josephine Charles akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji Miti.
Waziri wa Elimu Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Rosemary Revocatus akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji Miti.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka akipanda Mti.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Mipango,Fedha na Utawala Michael Henerico akipanda Mti.
Msimamizi wa Mazingira Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Josepheni Charles akipanda Mti.
Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akipanda Mti.
Mhfadhi wa Mambo ya Kale mkoani Shinyanga chini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)Wile Shuli akipanda Mti.
Zoezi la Upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la Upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la Upandaji Miti likiendelea.
Zoezi la Upandaji Miti likiendelea.
Awali viongozi wakiwasili eneo la upandaji Miti katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Wadau mbalimbali wa Mazingira wakiwasili eneo la upandaji Miti katika Chuo Cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Picha ya Pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Post a Comment

0 Comments