Header Ads Widget

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO NA MANISPAA YA SHINYANGA,WAMETEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII,KUUNGA JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUHAMASISHA UTALII HAPA NCHINI

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO NA MANISPAA YA SHINYANGA,WAMETEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII,KUUNGA JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUHAMASISHA UTALII HAPA NCHINI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
CHUO cha Sayansi za Afya Kolandoto na Manispaa ya Shinyanga, wametembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo katika Manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka Mitatu ya Rais Samia Madarakani,pamoja na kuunga Juhudi zake za kuhamasisha Utalii hapa Nchini.

Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 11,2024 kwa kutembelea baadhi ya Vivutio vya Utalii vilivyopo Manispaa ya Shinyanga, ambapo kuna Vivutio 13 vilivyopitishwa na Bodi ya Utalii Tanzania.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka akizunguma kwenye ziara hiyo,amesema wao kama Taasisi inayojishughulisha na Masuala ya Afya, wamekuwa wakimuunga Mkono Rais Samia katika Sekta mbalimbali, na kwamba ndani ya miaka Minne Mfululizo wameshatembelea karibu Mbuga zote za Wanyama hapa nchini, ikiwamo na kupanda Mlima Kilimanjaro.

“Chuo chetu cha Sayansi za Afya Kolandoto tuna mkubali sana Rais Samia kwa utendaji wake kazi na hasa Sekta hii ya Afya ameitendea haki na kuleta mapinduzi makubwa, ndiyo maana tuna Muunga Mkono pia katika Sekta ya Utalii(The Royal Tour), hakuna Mbuga ambayo hatujafika na tumekwenda kutalii hadi Zanzibar, yote hii ni kuunga Juhudi za Rais Samia kuhamasisha Utalii,”Amesema Shiluka.
Naye Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga, amesema katika Manispaa hiyo kuna jumla ya Vivutio vya Utalii 13, lakini katika ziara hiyo wametembelea Vinne, huku akitoa wito kwa wananchi wa Shinyanga watembelee Vivutio hivyo, ili kuunga juhudi za Rais Samia kuhamasisha Utalii.

Amesema Sekta ya Utalii imekuwa na Mchango Mkubwa katika kuchangia Pato la Taifa, na kumpongeza Rais Samia kwa kuhamasisha Utalii hapa Nchini.
Aidha, katika ziara hiyo Vivutio vya Utalii ambavyo vimetembelewa ni kuona Chemchem ambayo inatoa Maji ya Moto iliyopo Uzogore, ambapo Maji yake ukiyatumia unaondoa Mikosi Mbalimbali, na kuna ushuhuda mwanamke ambaye alikuwa Tasa alipotumia maji hayo alipata Mtoto.

Vivutio vingine vilivyotembelewa ni eneo la Makumbusho Mazingira Center, eneo jingine ni Mahali ambapo Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipowahutubia Watanzania wakati wa kudai Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Eneo jingine ni Mahali ambapo Bendera ya Mkoloni Mwingereza ilipotelemshwa na kupandishwa Bendera ya Tanganyika mara baada ya kupata Uhuru, pamoja na kutembelea pia Makaburi 8 ya wapiganaji wa Jeshi la Kiloloni yaliyopo Mlima wa Oldshinyanga.

TAZAMA PICHA ZA VIVUTIO VYA UTALII 👇👇
Eneo la Kivutio cha Utalii ambalo ni Chemchem yenye Maji ya Moto lipo Uzogore.
Mahali ambapo Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipowahutubia Watanzania wakati wa kudai Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Mahali ambapo Bendera ya Mkoloni Mwingereza ilipotelemshwa na kupandishwa Bendera ya Tanganyika mara baada ya kupata Uhuru.
Moja ya Kaburi wa Wanajeshi wa Kikoloni Kati ya Nane ambao walizikwa katika Mlima wa Oldshinyanga.
Ziara ya kutembelea Vivutio vya Utalii katika Manispaa ya Shinyanga ikiendelea.

Post a Comment

0 Comments