Header Ads Widget

UMUHIMU WA WAZAZI NA WALIMU KUTUMIA ZANA ZA KUJIFUNZIA KUWAFUNDISHA WATOTO

 UMUHIMU WA WAZAZI NA WALIMU KUTUMIA ZANA ZA KUJIFUNZIA KUWAFUNDISHA WATOTO

Na Tonny Alphonce, Mwanza

Zana za kujifunzia na kufundishia huwakilisha vifaa vyote ambavyo mwalimu hutayarisha na kutumia wakati wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili zimrahisishie ufundishaji wake na kuwafanya wanafunzi waelewe somo kirahisi zaidi.


Mwalimu anapotumia zana mwanafunzi hupata faida kwa kujifunza zaidi  kwa kuona ,kugusa, kuonja,kunusa na kusikia kwa kutumia njia hii mtoto hufurahia somo pia humpatia mtoto maarifa na ujuzi kwa njia ya mkato na ujuzi wa maarifa hayo huwa vigumu kusahaulika upesi.

Pamoja na faida hizo kumekuwa na tatizo la wazazi kushiriki  katika kutengeneza zana hizo za kujifunzia watoto ambapo baadhi ya wazazi hukwepa wakidhani ni gharama kubwa kuandaa zana hizi ambazo kiuhalisia hutengenezwa na malighafi zilizopo katika mazingira yao yanayowazunguka.

Shirika la Tanzania Eary Childhood Education and Care -TECEC kwa kushirikiana na walimu wa madarasa ya awali katika shule ya  msingi ya Luchelele pamoja na wazazi wameunda  zana na vifaa vya kujifunzia na kuchezea kwa watoto wa darasa la awali kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira ya shule.

(PICHA) Walimu wa madarasa ya awali katika shule ya  msingi ya Luchelele, Wazazi na Wanafunzi wakishiriki kutengeneza zana na vifaa vya kujifunzia na kuchezea watoto.

Mkurugenzi wa TECEC Joel Elphas anasema wao kama shirika wanajua umuhimu watoto  kujifunza na kucheza na kupitia Zana mbalimbali za kujifunzia kutaweza kukuza ujuzi wao wa kijamii, kiakili, kimwili na kihisia.

Joel amesema kupitia vifaa hivyo vya ubunifu vinatoa uhakika kwa watoto kupata fursa ya kujifunza kwa njia ya vitendo na kujifurahisha, wakati pia wakichunguza mazingira yao ya karibu.

“Mwanzoni ilikuwa ngumu kuwapata wazazi ili nao washiriki katika utengenezaji wa zana hizi lakini baada ya kuwaelimisha tumepata ushirikiano mkubwa na tumefikia lengo kama taasisi kutengeneza zana nyingi ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa vijana”.alisema Joel

Amesema wanajivunia kuwa sehemu ya juhudi hizo za kipekee kwa kuwa zimewezesha upatikanaji wa elimu bora na fursa za kujifunza kwa watoto  na amewashukuru  walimu wa madarasa ya awali, wazazi na walezi kwa mchango wao mkubwa na ushirikiano wao katika kufanikisha mradi huo wa kutengeneza zana za kujifunzia.

Joel amewataka wazazi kujenga utamaduni wa kutengeneza zana za kujifunzia wao pamoja watoto wao kwa kuwa malighafi zote zinapatikana katika mazingira waliyopo na kama watahitaji msaada wa kiufundi wanaweza kuwasiliana na shirika la TECEC kwa msaada zaidi.

Ester Macha  ambaye ni mtaalamu wa elimu ya awali kutoka TECEC amesema kuwa katika kutekeleza zoezi hilo wazazi  na wanafunzi walishirikishwa ili kutoa mawazo yao na michango yao ya ubunifu na kwa pamoja wakafanikiwa kutengeneza zana za kujifunza ambazo zilikuwa rahisi kwa watoto kuelewa na kufurahia ujifunzaji shuleni.

“Tulibaini kwamba vifaa kama vile chupa za plastiki, maboksi,Sponji na vitu vingine vya kawaida vinaweza kutumiwa kutengeneza zana hizi za kuchezea na kujifunza zikiwa zinahitaji ubunifu bila gharama kubwa kwa kuwa  rasilimali zote zipo kinachohitajika ni kutengeneza tu vifaa hivyo”.alisema Ester

Mwalimu wa darasa la awali  Zawadi Kokutangilila amesema ni vema wazazi na walimu kupewa  ujuzi wa namna ya kutengeneza zana za kufundishia kwa watoto wa madarasa ya awali kwa sababu itasaidia mtoto kuelewa kwa urahisi kwa kuwa shuleni atafundishwa kwa kutumia Zana na akirudi nyumbani atafundishwa na mzazi kwa kutumia tena Zana zilizopo nyumbani.

Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Mwalimu Martin Nkwabi amesema madarasa ya awali kwa mwongozo uliopo yanatakiwa kuwa na vifaa vingi vya kuchezea watoto lakini vifaa hivyo vinatakiwa viendane na kujifunza.

Mwalimu Martin amesema ndio maana wanasisitiza katika madarasa ya awali ni vema walimu wakatumia Zana zaidi katika kufundishia ili watoto wapate uelewa zaidi wa kile mwalimu alichokusudia kukifundisha.


“Mwanafunzi wa darasa la awali tukumbuke anafundishwa vitu vidogo vidogo kama kushirikiana na wenzake,kujifunza lugha na kufundishwa kwa njia ya picha hayo ndio malengo ya elimu ya awali”.alisema Mwl Nkwabi

Akizungumzia umuhimu wa utengenezaji wa Zana kwaajili ya kufundishia watoto,Mwl Nkwabi amesema walimu wamekuwa wakipewa elimu ya namna ya utengenezaji wa Zana kwa kushirikiana na mashirika yanayotekeleza afua za watoto.

Nao wazazi Joel Mafuru na Agness Masanja  ambao wamewahi kupewa elimu ya utengenezaji wa Zana wamesema mwanzoni hakuwakujua kama zana hizo ni muhimu katika ujifunzaji wa mtoto lakini wameshuhudia jinsi watoto walivyochangamka na kupata furaha wanapojifunza kupitia zana hizo.

“Kwa sasa ninao uwezo wa kutengeneza zana hizi na kuanzia na nimefanikiwa kumtengenezea mwanangu Zana mbalimbali ambazo zinamsaidia katika safari yake hii ya masomo ya darasa la awali”.alisema Mafuru

Kanuni za vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na watoto wachanga ya mwaka 2012 inahusisha mchakato  wa uandaaji wa kiongozi cha utengenezaji wa vifaa vya michezo na kujifunzia watoto chini ya miaka 5.

Vilevile, uelewa juu ya umuhimu wa ujifunzaji kupitia michezo haukupewa kipaumbele katika ngazi zote za maamuzi, udhibiti ubora, watoa huduma, waelimishaji na jamii kwa ujumla ikiwemo wazazi.

Ukosefu wa vifaa vya kuchezea watoto, vitabu, uelewa na ujuzi kuhusu malezi na wazazi kutokuchangamana na watoto mara kwa mara nayo imeripotiwa kama changamoto 

Pia Program  Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maeldeleo ya Awali ya Mtoto Mwenye umri kati ya miaka 0-8 ,inasisistiza juu ya maazingira rafiki na shawishi ya mtoto kujifunzia ili kuufanya ubongo wa mtoto uende sambamba na umri wake,huu ni umri unaoamua hatma ya mtoto baada ya kuvuka umri wa miaka nane huku tafiti na wataalam wakisema kesho ya mtu inaanza kujengwa kwenye umri kati ya miaka 0-8. ndio maana


Post a Comment

0 Comments