Header Ads Widget

MKOA WA SIMIYU KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA AMREF TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI KUPITIA UFADHILI WA SERIKALI YA MAREKANI


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Boniface Maro (aliyesimama) wakati wa Mkutano wa tathimini wa robo ya kwanza ya mwaka wa mradi wa Afya Thabiti. Mradi huo unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania na timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mkoa ya Simiyu unalenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI nchini.
Wakili Mwanahamisi Kawega, akimwakilisha Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Bi Prisca Kayombo, Wakati wa Mkutano wa tathimini wa robo ya kwanza ya mwaka wa mradi wa Afya Thabiti, Mradi huo unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania na timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mkoa ya Simiyu unalenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI nchini.
Ernest Kisandu, Mwakilishi kutoka Ofisi va Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakati Mkutano wa tathimini wa robo ya kwanza ya mwaka wa mradi wa Afya Thabiti.


Dkt Rita Mutayoba, Mkurugenzi wa kiufundi wa Mradi wa Afya Thabiti, Amref Tanzania
Picha ya Pamoja wakati Mkutano wa tathimini wa robo ya kwanza ya mwaka wa mradi wa Afya Thabiti.






Simiyu, Tanzania - Februari 07-08, 2024




Shirika la Amref Health Africa, Tanzania kwa kushirikiana na Uongozi na timu za Afya za mkoa na halmashauri za Simiyu imefanya Mkutano wa tathimini wa robo ya kwanza ya mwaka wa mradi wa Afya Thabiti, mkutano huo wenye lengo la Kupokea taarifa ya utendaji wa kipindi cha robo mwaka wa kwanza (October-December 2023) wa mradi na Kujadili mafanikio, changamoto na mafunzo yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa mradi wa Afya Thabiti wenye lengo la kutoa huduma za VVU/UKIMWI katika mkoa wa Simiyu na Mara.



Mradi huo unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania na timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mkoa ya Simiyu unalenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI nchini.



Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na ulifunguliwa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Wakili Mwanahamisi Kawega, akimwakilisha Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Bi Prisca Kayombo.



Akizungumza na washiriki Wakili Kawega alisema, “Mkoa wa Simiyu umefanikiwa kufikia malengo matatu muhimu ya kimataifa ya 95:95:95 katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU. Lengo la kwanza la 95, ni kuhakikisha wananchi wenye maambukizi ya VVU wanatambua hali zao limefikiwa kwa asilimia 100.4%, ikilinganishwa na lengo la asilimia 95%. Lengo la pili la 95, kuwapa dawa wenye VVU limefikiwa kwa asilimia 96.7%, na lengo la tatu (95) la kuwahimiza watu hao kutumia dawa ili kufubaza virusi vya UKIMWI limefikiwa kwa asilimia 97.4%, ikilinganishwa na lengo la asilimia 95%”.



Hata hivyo, kuna kundi la vijana na watoto kuanzia umri wa miaka 0-24, ambalo bado halijafikia viwango vya kutambua hali zao za VVU na kutumia dawa. Ni muhimu kutoka na maadhimio ya jinsi ya kufikia kundi hili na kuwahimiza kutumia dawa. Aliongeza Wakili. Wakili Kawega



Akizungumza na washiriki, Wakili Kawega alisema, “Ni muhimu kutambua kwamba huu ni mradi muhimu na fursa kubwa, na hivyo basi ni wakati wa kutumia vyema mradi huu ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi zaidi wanafikiwa na kupata huduma zinazostahili”.



Ernest Kisandu, Mwakilishi kutoka Ofisi va Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesema Wizara itaendelea kutoa ushirkiano kwa Wadau mbalimbali wa kupambana na VVU na UKIMWI Nchini kusudi malengo mahusi ya kutokomeza VVU vaweze kutimia.



Kwa upande wake, Dkt Rita Mutayoba, Mkurugenzi wa kiufundi wa Mradi wa Afya Thabiti, Amref Tanzania alisema "Ushirikiano na uongozi kutoka katika utekelezaji wa mradi wa Afya Kamilifu uliomalizika Septemba 2023, umetuwezesha kufanikisha malengo tuliyokuwa nayo. Tunashukuru sana timu nzima ya mkoa na halmashauri kwa usimamizi wao madhubuti kuratibu huduma za VVU/UKIMWI mkoa wa Simiyu.



Ameongeza kwa ushirikiano na timu za afya za wilaya kwa pamoja tulifanya zoezi la kuthibitisha ama kusajili wateja wote kwa alama ya kidole kwa wale wote ambao wanapokea huduma za VVU katika vituo vyetu yaani zoezi la Bio-metric, "Tumeweza kufikia asilimia 92 ya malengo yetu na tunatarajia kufikia asilimia 100 kabisa. Lengo letu ni kuhakikisha tunawafikia walengwa wote na kuwapatia huduma sahihi", amesema Dr Rita Mutayoba, Mkurugenzi wa Kiufundi, Mradi wa Afya Thabiti.



Amref Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wizara zote, mashirika ya serikali, wafadhili, mashirika ya kijamii (CBOs), mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), sekta binafsi, na wanajamii. Katika kuchangia upatikanaji sawa na endelevu wa huduma bora za afya ya msingi (PHC) na hatimaye kuchangia katika kufanikisha huduma ya afya kwa wote (UHC) nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments