Header Ads Widget

WANANCHI NDEMBEZI WAMEJITOKEZA KUUSAKA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEZAMA MTO MHUMBU SIKU YA NNE SASA

WANANCHI NDEMBEZI WAMEJITOKEZA KUUSAKA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEZAMA MTO MHUMBU SIKU YA NNE SASA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WANANCHI wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wamejitokeza kuendelea kuusaka mwili wa Mwanafunzi Salumu Matheo (11), aliyekuwa akisoma darasa la Nne shule ya Msingi Bugoyi “B”,ambaye amedaiwa kufariki dunia wakati akivua Samaki katika Mto Mhumbu akiwa na wenzake watatu.
Tukio hilo limetokea Februari 4 , 2024 Majira ya saa 12 jioni, ambapo imepika siku ya Nne sasa mwili wa Mwanafunzi huyo bado haujaonekana, huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likisitisha kuusaka Mwili wa Mtoto huyo baada ya kufikisha Masaa 72, na sasa kazi iliyobaki ni wananchi kuusaka mwili huo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukaleli Japhet Kisusi akizungumza leo na waandishi wa habari, amesema baada ya Jeshi la Zimamoto na Uokojai kusitisha zoezi la kuusaka mwili wa Mtoto huyo, imebidi wananchi kuusaka wenyewe ambao umeshafikisha siku Nne ndani ya Maji na bado hawajaupata.
“Kwa Mujibu wa Jeshi la Zimamoto wao wanafanya kazi Masaa 72 yakiisha bila kuupata Mwili kazi ina baki ya Wananzengo, ndiyo maana unaona vijana wapo kwenye zoezi la kuusaka mwili wa Mtoto huyo kwa kuzama ndani ya maji,”amesema Kisusi.

Nao vijana ambao wamejitokeza kuusaka Mwili wa Mtoto huyo akiwamo Juma Ismail, wamesema tangu majira ya saa moja Asubuhi wapo kwenye Mto huo wakiusaka mwili kila kona, ikiwamo kufukua vifusi ambavyo vipo ndani ya maji na kukata miti ili kuona kama mwili utaibuka juu, lakini bado hawajafanikiwa kuupata.
“Leo ni Siku ya Nne Mwili wa Mtoto huyu upo ndani ya maji kwa kawaida ilipaswa mwili wake kuelea juu ya maji, lakini tumesaka hatujapata kitu itakuwa amenasa chini kwenye vifusi ndiyo maana tunafukua ili aibuke juu, na tutaendelea kumsaka hadi tutampata,”amesema Ismail.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Kata ya Ndembezi Solomon Najulwa "cheupe" amewapongeza wananchi wa Ndembezi kwa Uzalendo waliouonyesha na kujitokeza kuusaka Mwili wa Mtoto huyo Mtoni.

Naye Baba wa Mtoto huyo Matheo Peter, ameshukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kuusaka mwili wa mtoto wake, na kutoa wito kwa wazazi wawe makini na watoto wao hasa kipindi hiki cha Mvua nyingi, kwamba wasiende kucheza kwenye Mito wala kuvua Samaki.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Wananchi wakiendelea kuutafuta Mwili wa Mtoto huyo katika Mto Mhumbu.

Post a Comment

0 Comments