Header Ads Widget

JESHI LA ZIMAMOTO LAENDELEA KUUTAFUTA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEDAIWA KUZAMA MTO MHUMBU SHINYANGA

JESHI LA ZIMAMOTO LAENDELEA KUUTAFUTA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEDAIWA KUZAMA MTO MHUMBU SHINYANGA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Shinyanga, limeendelea kuutafuta Mwili wa Mwanafunzi Salumu Matheo (11) aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Bugoyi “B” Mkazi wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ambaye ameelezwa kufariki dunia kwa kuzama Mto Mhumbu akiwa na wenzake watatu walipokwenda kuvua Samaki na kuogelea.
Zoezi hilo la Uokoaji limechukua muda wa Siku Tatu, tangu kutokea tukio hilo la Mtoto kuzama Februari 4 mwaka huu Majira ya Saa 12 Jioni.

Sargent Masoud Mohamed akizungumza leo Februari 7, 2024 kwa Niaba ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga eneo la tukio katika Mto huo Mhumbu wakati wakiutafuta Mwili wa Mtoto huo amesema bado hawajaupata.
Amesema leo ni Siku ya Tatu wakiendelea kuutafuta Mwili wa Mtoto huyo bila Mafanikio, ambapo kwa taratibu mtu akizama Maji anapaswa siku ya tatu mwili wake kuibuka juu, lakini mwili wake bado haujaonekana na kwamba huenda amenasa sehemu chini ya mti ambao umeanguka ndani ya maji sababu wakiugusa mti huo kunatokea harafu kali, huku maji yakiendelea kujaa mtoni.

“Jeshi la Zimamoto na Uokoaji bado tunaendelea kuusaka Mwili wa Mtoto huyo na leo ni siku ya tatu tangu kuzama kwake na lipaswa awe ameshaibuka juu lakini bado haonekani huenda atakuwa amenasa na kitu chini ya maji,”amesema Mohamed.
Naye Mjomba wa Mtoto huyo Said Najimu, akielezea tukio hilo amesema siku hiyo Februari 4 akiwa na wenzake wakicheza alimuomba awafungulie TV ili waangalie Mpira , na wakati akiendea kuwa washia ghafla umeme ulikata, ndipo wakatoroka na kwenda kuvua Samaki na kuogelea katika Mto huo.

Anasema ilipofika Majira ya saa Moja jioni ndipo wenzake wakaja na kutoa taarifa kwamba Rafiki yao amezama Mtoni, na kuchukua jukumu la kwenda kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuwapatia msaada wa kumtafuta.
Anasema walipofika eneo la tukio walikuta nguo zake pamoja na Yebo, lakini mwili wake wameutafuta hadi leo bila ya mafanikio.

Naye Mmoja wa waokoaji John Mwandu, amesema katika utafutaji mwili wa Mwanafunzi huyo, walipata Mwili wa Mtoto mwingine wa jinsia ya kike ambao wameupeleka chumba cha kuhifadhia Maiti Hospitali Manispaa ya Shinyanga kwa utambuzi wa wazazi wake.
Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Kalugole Ramadhani, ametoa wito kwa wazazi kwamba kipindi hiki cha Mvua kubwa pamoja na Mito kujaa Maji, wasiruhusu watoto wao kwenda kuvua Samaki wala kuogelea sababu mito hiyo imekuwa na kina kirefu.

TAZAMA PICHA ZA MAOKOZI HAPA CHINI👇👇
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga wakiendelea na zoezi la kutafuta Mwili wa Mwanafunzi Salumu Matheo aliyedaiwa kuzama katika Mto Mhumbu.

Post a Comment

0 Comments