Header Ads Widget

RC MNDEME AIPONGEZA HALMASHAURI YA KISHAPU KUPATA HATI SAFI, YAJIBU HOJA VIZURI ZA CAG

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu leo Tarehe 23 Juni 2023 limefanya Mkutano Maalumu wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 unaoisha 31 Juni 2023.

Awali Mweka Hazina wa Halmashauri Ndugu. Georgy Sulumbwealitoa taarifa fupi juu ya hoja zinazoikabili Halmashauri ambayo alieleza kuwa katika ukaguzi wa 2021/2022 Halmashauri ilitunukiwa hati safi ikiwa na jumla ya hoja 54 kati ya hizo 22 zimefungwa na 32 zipo katika hatua ya utekelezaji
Katika Baraza hilo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) zinazoonesha alikagua hesabu za Serikali za Halmashauri na kutoa Hati safi ya ukaguzi.

“Mhe. Mwenyekiti nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye ametupa kibali cha kuwa mahali hapa, Mhe, Mwenyekiti nitumie furusa hii kuwapongeza kwa kupata Hati Safi katika taarifa ya CAG tunayoijadili leo nyinyi mko safi rai yangu kwenu muendelee kupata hata hii safi mwisho wa ukaguzi huu ni mwanzo wa ukaguzi mwingine msipate hati ya mashaka au hati chafu, haya mazuri mnayoyapa ni kwaajili ya ushirikiano mzuri mlionao kati ya Madiwani na Wataalamu ushirikiano huu uendelee.” Alisema Mndeme
Pia ameitaka Halmashauri iongeze kasi ya ukusanyaji Mapato kwa siku hizi Saba zilizobakia kabla ya kufunga Mwaka wa Fedha 2022/2023 ili kufikia lengo la Asilimia 100 ya Ukusanyaji wa Mapato

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson Amemwahidi Mkuu wa Mkoa kutekeleza Maagizo na Maelekezo yote yaliyotolewa kuanzia kwenye kamati ya Fedha, Kamati ya Ukaguzi
“Mhe. Mwenyekiti nichukue furusa hii kwanza nishukuru Baraza lako tumefanya kazi kubwa sana yakisheria ambayo tulipaswa kuifanya leo, Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu naomba kutoa ahadi kwako kwamba tutahakikisha maagizo na maeelekezo yote yaliyotolewa kuanzia kamati ya Fedha na Mkaguzi wa Serikali pamoja na Viongozi tutayasimamia kikamilifu ili kuhakikisha Halmashauri yetu inapunguza hoja.
 Pia nichukue furusa hii kipekee kumshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupendezwa kuniamini kuendelea kubaki katika Halmashauri hii, Hii inatokana na ushirikiano mkubwa wa Madawani katika kufanya kazi “amesema Johnson
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude, Amesema kuwa ataendelea kutoa Ushirikiano mkubwa kwa Baraza la Madiwani katika usimamizi wa ukusanyaji wa Mapato ili kuhakikisha Halmashauri kuwa na Hati safi kila Mwaka wa Fedha.
Aidha Mkuu wa Mkoa Ameitaka Halmashuri kubuni zaidi vyanzo vya Mapato amabavyo vitaifanya Halmashuri kuwa na Mapato Makubwa.

Post a Comment

0 Comments