Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUPANDA MITI ILI KUONDOKA NA UKAME WA MVUA

Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomoni Najulwa akipanda mti katika viwanja vilivyokaribu na ofisi yake akiwa pamoja na wadau wake mbalimbali
Suzy Luhende, Shinyanga Blog

Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa amewataka wananchi wote wanaoishi mtaa wa Dome kupanda miti ya matunda na ya kivuli katika maeneo wanayoishi ili kuondokana na ukame wa mvua unaosababishwa na kukosekana kwa miti.

Agizo hilo amelitoa leo wakati walengwa wa mfuko wa Tasaf na wananchi wengine wakipanda miti katika viwanja vilivyokaribu na ofisi ya mtaa wa Dome ambapo amepanda miti 1200 na kuwataka wananchi wa mtaa huo kupanda miti angalau kila familia ipande miti mitano.

Najulwa ambaye aliungana na viongozi wa dini mbalimbali wa mtaa huo kupanda miti na kuiombea ili isitawi vizuri amesema atahakikisha miti hiyo anaitunza na kuilinda isishambuliwe na mifugo ili iweze kukua isaidie vizazi vijazo na vilivyopo kwa sasa. 

"Miti hii tunayopanda leo itasaidia watoto na watu wazima kujipatia matunda  na hapa tunapopapanda watakuja watu mbalimbali maharusi kupigia picha kwa sababu itakuwa mahali pazuri pa kupendeza na kutakuwa na hewa nzuri kila mmoja atatamani kupata hewa ya hapa, hivyo niwaombe na wananchi mpande miti kwa wingi majumbani kwenu ili kwa baadae mje mfaidike nayo"amesema Najulwa 

Zoezi hilo la upandaji lilisimamiwa na afisa misitu wa manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga ambaye alikuwa anatoa maelekezo ya upandaji miti na kutoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi wa mtaa huo ambapo amesema miti inasaidia mvua kunyesha na miti ya matunda kupata matunda.

"Sisi ni wahanga wa mabadiliko ya tabia nchi, ili mabadiliko haya yasiendelee kuwepo tunatakiwa tupande miti kwani ardhi yetu inahitaji maji ya kutosha, kwani mtu mmoja ili aweze kupata hewa anahitaji miti 15, hivyo tunatakiwa kupanda miti, kwani upepo wa mvua unapovuma unasafirisha mawingu unaelekea kwa yule aliyepanda miti, na mvua ndogo haiwezi kuingia chini kwani inakimbilia kwenye mitaro na kwenda kwenye mito,"amesema Manjerenga.

Manjerenga amesema changamoto inayojitokeza kwa wananchi ni mapokeo kwani mtu anajiuliza kuwa atanufaika na matunda hayo baada ya miaka mitano ama  10 anaona ni mbali sana kumbe ni mda mchache, pia mbuzi wanafugwa ndani wanakula wali, mchele wanafunua masufulia, hivyo wanakuwa wasumbufu kwa watu wengine na sheria zinasema unapogawiwa eneo hutakiwi kumbuguza jirani yako.

"Hivyo wajibu wangu ni kutoa elimu ya upandaji miti, ndiyo maana tumeleta miti, mbolea na mchanga katika mtaa huu  na kutoa elimu kwa jamii na tunaomba kila kaya ipande miti mitano mitatu ya matunda na miwili ya kivuli na kuhakikisha tunaitunza miti mimi nawakalibisha mje mchukue," amesisitiza Manjerenga.

Manjerenga amesema takwimu zinaonyesha kuwa imekuwa ikipandwa miti 100 miti inayopona ni 16 tu inapona,  hivyo mradi huu wa miti waitunze ili miti yote waliyoipanda ipone yote usiwepo wa kuishia njiani.

kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Balina William Lameck amesema mradi huo ni mzuri utasaidia mvua kunyesha na utasaidia watoto kujipatia matunda na kulinda afya, pia hata hewa itakuwa ni nzuri,  hivyo inatakiwa iitunzwe.

Baadhi ya walengwa wa mfuko wa  Tasaf mtaa wa Dome Lucia Masunga na Joseph Nkuba, waliokuwa wakipanda miti hiyo wamemshukru sana Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kuwakumbuka, wameahidi watashirikiana na mwenyekiti wao wa mtaa wa Dome katika kuitunza miti hiyo na watafuata miti kwa ajili ya kupanda majumbani kwao.




Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomoni Najulwa akizungumza na wananchi wa mtaa huo kabla ya kuanza kupanda miti


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Balina William Lameck akipanda mti
Mwalimu wa shule ya msingi Balina akipanda miti


Wadau mbali wakiwemo wachungaji wakipanda miti katika viw wa viwanja vya Dome

Afisa misiti manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga na Mwenyekiti wa Dome wakionyesha miti ya kupanda na kutoa maelekezo

Afisa misitu wa manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akipanda mti na kutoa maelezo jinsi ya kupanda miti hiyo

Afisa misiti manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga na Mwenyekiti wa Dome wakionyesha miti ya kupanda na kutoa maelekezo


Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi tawi la Ndembezi akizungumza kabla ya kupanda miti

Afisa misitu wa manispaa ya Shinyanga Ezra Majerenga akitoa maelezo jinsi ya kuitunza miti hiyo

Viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa mtaa wa Dome baada ya kuombea upandaji miti wakimsikiliza mwenyekiti wa mtaa wa Dome
Wanafunzi wa shule ya msingi Balina wakiwa wamebeba miti kwa ajili ya kupanda
Wakazi wa mtaa wa Dome wakiendelea kuchanganya mchanga wa kupandia miti


Wanafunzi wa shule ya sekondari Balina wakimsikiliza vizuri mwenyekiti akizingumza



Mzabuni wa kupanda miti akitoa maelezo kabla ya kupanda miti hiyo

Post a Comment

0 Comments