Header Ads Widget

MKURUGENZI MKUU RUWASA ATAKA WAKANDARASI MIRADI YA MAJI WENYE UZALENDO WAPEWE VYETI

Mkurugenzi mkuu  wa Ruwasa mhandisi Clement Kivegalo akiongea  kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji vijijini.

Na Kareny Masasy,  Shinyanga

MKURUGENZI  mkuu wa wakala  wa maji na usafi wa mazingira vijijini  (Ruwasa) Mhandisi Clement Kivegalo  amesema Makampuni  ya wakandarasi  wazalendo wanaotekeleza miradi ya maji nchini wenye kufanya vizuri wapewe cheti cha kutambuliwa na pongezi.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 13/07/2023 kwenye ziara yake mkoani hapa alipotembelea utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Samuyenakukagua ujenzi wa  tanki  la maji lenye ujazo  wa lita 100,000 na mnara wa mita 12.

Mhandisi Kivegalo amesema mradi wa maji unaotekelezwa kijiji cha Ishinabulandi  umefikia asilimia 37 unaenda vizuri hivyo mkandarasi wa kampuni ya  Mbesso Construction  hajachukua fedha ya serikali yoyote mpaka sasa ametumia yakwake.

Mhandisi Kivegalo amesema wakandarasi wa namna hiyo  ni wazalendo ofisi za Ruwasa mkoa  ziwaandalie  cheti cha pongezi na chakumtambua ili anapoomba tena kazi aweze kufahamika nakupewa tena.

Mhandis Kivegalo amewapongeza Ruwasa mkoa na wilaya kwa kazi nzuri wanazozifanya  sanjari na  jumuiya ya watumia maji (CBWSO )iliyopo kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu kwa kuwa na ofisi na ukusanyaji mzuri wa mapato.

Mhandisi Benjamin Pares msimamizi wa kampuni hiyo ameomba kuongezwa muda kwa kuchelewa kuanza  kazi huku changamoto  akieleza ni ucheleweshaji wa kupata vifaa  ikiwa asilimia kubwa anatumia mabomba na unatarajia kukamilia mwezi Februari mwaka huu.

Meneja wa Ruwasa  wilaya ya Shinyanga  Mhandisi Emaeli Nkopi amesema  mradi huo unatarajia kuhudumia vijiji nane ambavyo ni   Ishinabulandi,Idodoma,Isela.Ibingo.Ng’wahalanga,Mwamala na Ibanza.

“Mradi huo unagharimu sh Billioni 4.7 ambapo kunajengwa  matanki mawili  moja Ishinabulandi na lingine kata ya Mwamala lenye ujazo wa lita 200,000 nakuhudumia watu 23,000.

Mwenyekiti wa jumuiya ya watumiaji maji  Kassimu Kishiwa  amesema mradi huo umewasaidia  hata baadhi ya akina mama kwenye familia ndoa zao kudumu kwani walikuwa  wanatafuta maji  nakuachika.

  Mtendaji wa jumuiya hiyo Hassan Alfan amesema wanahudumia vijiji  15  na mafanikio mpaka sasa  wamejenga kituo cha kutolea maji kwa fedha za makusanyo  na ofisi ya Ruwasa wilaya ya Kishapu iliwakabidhi pikipiki mbili

Mkurugenzi  mkuu wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa  Mhandis Clement  Kivegalo akiongea kwenye  kikoa na   jumuiya za watumia maji Kishapu. wa maji Kishapu mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa nchini  Mhandisi Clement Kivegalo akiwa na meneja wa Ruwasa Mkoa Julieth  Payovera pamoja na meneja wilaya ya Kishapu Mhandis  Dickson Kamazima.
Wakwanza kushoto ni meneja  Ruwasa wilaya ya Shinyanga  Mhandisi Emael Nkopi  katikati ni  mkurugenzi mkuu wa Ruwasa nchini Mhandisi Clement Kivegalo na pembeni yake meneja Ruwasa mkoa wa Shinyanga   Mhandisi Julieth  Payovela.


Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa  Mhandisi Kivegalo akiongea na mhasibu wa watumia maji  Khamisa Thabiti  katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Masengwa  wilayani Shinyanga.

Tanki la maji linalojengwa  kijiji cha Ishinabulandi kata ya Masengwa lenye ujazo wa  lita 100,000

Post a Comment

0 Comments