Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BARRICK NORTH MARA WALIVYOPOKEA TUZO YA USHINDI WA MLIPA KODI WA KWANZA NCHINI TANZANIA


Baada ya kutunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Mlipa Bora na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kilele cha Wiki ya Mlipa Kodi iliyomalizika hivi karibuni,Wafanyakazi wa Mgodi wa Twiga Minerals wa Barrick North Mara, wamepokea taarifa hiyo kwa furaha na kulipokea kombe la ushindi lilipowasili mgodini hapo.

Twiga Minerals Corporation, inasimamia shughuli za: Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga; Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Tarime– pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi (Pangea) ambao pia upo Shinyanga ambao kwa sasa uko katika hali ya kufungwa.

Mnamo mwaka wa 2020, Twiga Minerals Corporation ililipa kodi ya mapato kiasi cha dola milioni $119, ambapo mwaka 2021, ililipa dola milioni $96.

Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliitambua Twiga kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya serikali kwa mwaka 2021. Kampuni yake tanzu - North Mara Gold Mine pia ilishinda tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa Wamiliki wa Leseni Maalumu za Uchimbaji katika Utekelezaji sera ya ushirikishwaji wazawa katika mnyororo wa uchumi wa madini (Local content) kwa mujibu wa Sheria ya Madini kifungu namba 123 mnamo mwaka 2021.

Akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha robo mwaka kwa vyombo vya habari mwezi Oktoba, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation Dk, Mark Bristow, alisema kuwa Twiga imechangia kwa zaidi ya dola bilioni 2.187 katika uchumi tangu mwaka 2019. Kati ya hizo, dola milioni 878 zililipwa katika mfumo wa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.
Kuhusiana na kusaidia biashara za ndani, Dk. Bristow alisema kuwa asilimia 80% ya manunuzi yenye thamani ya kiasi cha dola bilioni $ 1.025 yalikuwa ya bidhaa za ndani.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo

Post a Comment

0 Comments