Header Ads Widget

YWL YAUNDA JUKWAA LA WANAWAKE KIJIJI CHA ICHONGO,YAWASAA WANAWAKE KUTOA TAARIFA ZA UKATILI

Mratibu wa Shirika la Young Women Leader ship Veronika Masawe 



Suzy Luhende,Shinyanga blog

Mratibu wa Shirika la Young Women Leadership(YWL), Veronika Masawe  amewataka wanawake wa kijiji cha Ichongo kata ya Iselamagazi halmashauri ya Shinyanga  kutoa taarifa za ukatili pindi wanapoona mtoto ama mwanamke akifanyiwa ukatili, ikiwa ni pamoja na kujitoa katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye familia zao.

Hayo ameyasema baada ya kuzindua rasmi jukwaa la wanawake na kuchagua viongozi wa jukwaa hilo, lililofanyika  katika kijiji cha Ichongo, ambapo amesema wanawake wanatakiwa kutoka kwenye ujima na kujitambua  na kuweza kutetea wanawake na watoto wanaofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali na watu ama na wenza wao.

Masawe amesema lengo la kuanzisha jukwaa hilo, ni kuwajengea uwezo ili wawe na mabadiliko na waweze kupaza sauti kwa kutetea haki ya wanawake na watoto wanaofanyiwa ukatili, pamoja na kuwa na maamzi mazuri katika familia zao na kuwa wajasili katika kutatua jambo, kwa kuwa jukwaa ni chombo shirikishi kinachotetea haki ya wanawake. 

"Nawaomba mjitoe katika kutetea wanawake  wenzenu  wanaofanyiwa ukatili na waume zao ikiwa ni pamoja na kutetea watoto wanaofanyiwa ukatili, mkijisimamia vizuri wanawake ukatili utapungua, hivyo mnapoona mtu anafanyiwa ukatili msinyamaze kimya kwa kuogopa toeni taarifa ili anaefanyiwa ukatili asaidiwe kwa wakati,"amesema Masawe.

Kwa upande wake afisa maendeleo wa kata ya Iselamagazi Joyce Sawala  amesema kazi ya jukwaa ni kutetea haki ya wanawake wanaofanyiwa ukatili. na kuwajengea mwongozo wa kuweza kuingia kwenye vikundi na kuondokana na dhamira potofu, ikiwa ni ni pamoja na kuwaunganisha kuingia kwenye mikopo ya halmashauri ambayo haina riba.

"Kiongozi anayechagukiwa anatakiwa awe mwadilifu na mchapakazi awe na ujasili wa kutetea wanawake wenzake wanapofanyiwa ukatili, kwani kuna baadhi yao wanauziwa chakula ndani kinaisha na kubaki familia ikilia njaa lakini mwanamke hana lakusema, lakini kama wanawake mtakuwa wajasiri mtashirikiana kwa pamoja ili chakula kisiuzwe,"amesema Sawala.

Viongozi wa jukwaa la wanawake waliochaguliwa Mwenyekiti ni Mary Sanga, na makamu wake ni Veronica Charles, katibu ni Christina Piter na katibu msaidizi ni Restuta Charles, na
Mweka hazina ni Nuru Hassan.

Baada ya kuchaguliwa mwenyekiti la jukwaa hilo Mary Sanga aliwataka wanawake wawe wajasili, na elimu waliyoipata wakawape na wanawake wenzao ambao hawakufika kwenye jukwaa hilo wasinyamaze kimya kila mwenye jirani afikishe ujumbe huu ili wanawake na watoto wawe salama 
Wanawake wa kijiji cha Ichongo wakiwa kwenye kikao cha jukwaa la wanawake

Viongozi wa jukwaa la wanawake waliochaguliwa

Mratibu wa Shirika la Young Women Leader ship Veronika  akizungumza na wanawake wakijiji cha Ichongo

Afisa maendeleo wa kata ya Iselamagazi Joyce Sawala akielezea sifaza kiongozi kwa wanawake

Wanawake wakifurahia jambo baada ya kumaliza uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la wanawake


Wanawake wakimsikiliza mratibu wa Mratibu wa Shirika la Young Women Leader ship Veronika Masawe

Post a Comment

0 Comments