Header Ads Widget

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA SHINYANGA BENARD SHIGELA ATOA MSAADA KITUO CHA BUHANGIJAMjumbe wa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Benard Reuben Shigela akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu mbalimbali katika shule ya Buhangija Manispaa ya Shinyanga

Suzy Luhende, Shinyanga blog

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Benard Reuben Shigela ametoa msaada wa chakula, vinywaji na pesa  katika kituo cha kulelea watoto  wenye mahitaji maalumu Buhangija.

Msaada huo ameutoa leo 25,2022 baada ya kutembelea shuleni hapo na kuwajulia hali baada ya kutokewa na ajali ya moto iliyosababisha kifo cha wanafunzi watatu walioteketea kwa moto ambao mpaka sasa haujafahamika chanzo chake.

"Nimefika hapa kuwatia moyo na kuwajulia hali zenu, pia nina chakula kidogo na vinywaji ambavyo Mungu amenijalia nigawane nanyi zitawasaidia kwa siku hizi, kinachotakiwa msihudhunike sana mtegemeeni Mungu siku zote za maisha yenu na msome kwa bidii, ili muweze kufaulu na kutimiza ndoto zenu,"amesema Shigela.

"Pia nawaomba wazazi wote na walezi  muwe na subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,  kwani serikali na uongozi wa shule inaendelea na ufumbuzi wa tatizo hili,"amesema Shigela.Post a Comment

0 Comments