Header Ads Widget

SHIRIKA LA YAWE LAWAFIKIA WANANCHI VIJIJINI KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI


                 Wakazi wa Kata ya Nyida wakipatiwa elimu juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. 

                Afisa mradi wa Shirika la YAWE Deus Lyakisi akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyida.

Na Shinyanga Press Club Blog

Shirika la YAWE la mjini Shinyanga limeanza kutoa elimu kwa jamii juu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika Kata za Halmashauri ya Shinyanga ,ili kuiwezesha jamii kuwa na uelewa na kuwafichuwa watu wanaofanya vitendo hivyo kutokana na kukiuka haki za binadamu.

Akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyida katika shule ya Msingi Nyida afisa mradi kutoka Shirika la YAWE Deus Lyakisi amesema wamelenga kutoa elimu ya kupinga ukatili kwenye jamii na shuleni kupitia mradi wa Keeping school children safe in Shinyanga utakao tekelezwa Kata ya Nyida, Didia na Puni kwa ufadhili wa mfuko wa wanawake Tanzania (WFT).

Lyakisi amesema lengo ni kuboresha maisha ya watoto shuleni na kuwa katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kupatiwa mbinu bora za kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Amesema wanalenga kuona mimba na ndoa za utotoni zinapungua au kuisha, watoto kujitambua na kufanya maamuzi sahihi na kuripoti kesi za ukatili,jamii kutowatelekeza watoto na walimu kuchukuwa jitihada za kushughulikia kesi za ukatili ili kukomesha matukio hayo.

Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nyida wamesema matukio ya ukatili wa kijinsia bado ni changamoto kubwa kutokana na kuendelea kutokea katika maeneo mbalimbali na kuiomba serikali kwa kushirikiana na wadau wa kupinga vitendo vya ukatili kuendelea kutoa elimu.

Kwa upande wake Amos Kadilana mkazi mkazi wa Nyida amekiri baadhi ya wanaume kufanyiwa vitendo vya ukatili na wake zao lakini wamekuwa wakiona aibu kutoa taarifa kutokana na hofu ya kuchekwa jambo ambalo linaendelea kuwaumiza wengi na kurudisha nyuma jitihada za kupambana na vitendo hivyo.

 

                                                                              
                     Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya msingi Nyida Julius Mwakalebela akiwaomba wananchi kushiriki katika vikao vya shule ili kutatua changamoto zinazowakabili watoto na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
        

     Afisa mradi Shirika la YAWE akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wananchi wa Kata ya Nyida.                     
                       Devota David Mwalimu wa malezi shule ya msingi Nyida akizungumza kwenye kikao 
                     Flora Masunga mkazi wa Nyida akizungumza kwenye kikao 
 Mkutano unaendelea                                

Post a Comment

0 Comments