Header Ads Widget

MALALAMIKO 5575 YA WANANCHI WALIOFANYIWA MADHIRA KATIKA MGODI WA ALMASI WA WDL MWADUI KUANZA KUSHUGHULIKIWA NA BARAZA HURU


Mkurugenzi mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy akimkabidhi katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa kushughulikia malalamiko ya wananchi waliofanyiwa madhira.

Suzy Luhende,SHINYANGA.

MKUU wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amelitaka baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi waliofanyiwa vitendo vya ukiukwaji wa kibinadamu katika mgodi wa almasi Mwadui Williamson Diamond Limited (WDL), ulioko wilayani Kishapu kufanya kazi kwa weledi na kutenda haki kwa walofanyiwa madhira.

Hayo ameyasema leo 29,2022 wakati akizindua baraza huru la kutatua na kupokea malalamiko ya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa Williamson Diamond limited (WDL) kuanzia mwaka 2009 hadi mai 2021.uzinfuzi uliofanyika mjini Shinyanga

Mkude amelitaka baraza hilo lililozinduliwa lifanye kazi kwa weledi kwa kutenda haki ya kila mwananchi wa chini aliyefanyiwa madhira mbalimbali na malalamiko yote ya walengwa yatendewe haki.

"Baraza hili tulilolizindua leo tumelipokea, tuendelee kushirikiana, pale litakapotokea tatizo baraza msisite kuleta ngazi ya wilaya ama ngazi ya mkoa ili litatuliwe kwa wakati, kwani sisi tunahitaji haki itendeke kwa walengwa wenyewe, na tunaamini mtatumia weledi wenu kama jopo katika kutenda utu kupitia wananchi,"alisema Mkude.


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya alisema siku hii waliisubiri kwa hamu na leo imetimia hivyo ameliomba baraza hilo wakafanye kazi kwa kutenda haki na pindi wakihitaji msaada utolewe kwa wakati, ili malalamiko yaliyopo yafanyiwe kazi kwa wakati.


"Hii siku tuliisubiri kwa hamu sana hakika hii ni serikali inayowapenda wananchi wake, pia tunaushukuru uongozi wa mkoa kwa kutusapoti, wananchi wametoa maoni yao wakiwa huru na madiwani walikuwa bega kwa bega na tume ya waanzilishi, hivyo tunaomba kazi iendelee,"alisema Jijimya.


Mwenyekiti wa baraza huru la usuluhishi Dr. Rugemeleza Nshala alisema baraza hilo lililoundwa sio la wafanyakazi wa Petra ama wa serikali, ni wafanyakazi huru kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya wananchi yaliyofunguliwa na yatakayofunguliwa ambapo kwa sasa kuna malalamiko 5575 ambayo yanatakiwa yahakikiwe ili yashughulikiwe.


"Timu yetu ina wanasheria ambao watasimamia malalamiko na kujua vitu gani vilikosewa, na katika timu hii waamzi wapo wanne ambapo ripoti zote zitawekwa katika mtandao wa Petra Diamonds na Williamson Diamonds Limited (WDL) na timu hii inaongozwa na kanuni ya haki na msingi unaoongoza ni utu na maridhiano,"alisema Nshala.


"Vijiji 12 wametembelea na kukutana na watu ambao umeongozwa na kanuni za umoja wa mataifa, ambalo kwa sasa serikali imeridhia uwepo wa baraza hilo na limezinduliwa leo kwa ajili ya kuanza kazi, ofisi itakuwa Shinyanga mjini kwa muda wa miezi minne na baadae ofisi itahamishiwa katika kijiji cha utemini wilayani Kishapu,"alisema Nshala.


Aidha mkurugenzi mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy amewashukuru viongozi wote ngazi ya kata hadi Taifa pia amelitaka baraza huru litekeleze majukumu yake vizuri ili kuhakikisha haki ya kila upande inaonekana.


Simon Mutinda ambaye ni mdau wa kampuni ya kimataifa (Partner_ prikwater House cooper)alisema watahakikisha jamii imepata suruhisho na kuhakikisha jamii inajimudu kiuchumi kwa sababu imeridhia kuwepo kwa baraza huru, hivyo litadumu kwa muda mrefu kwa ajili ya kushughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi.



Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo alishukuru kwa kuundwa baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi, hivyo alitaka baraza hilo lisimamie haki ya wananchi wote waliofanyiwa madhira mbalimbali waliofanyiwa ndani ya mgodi wa (WDL).


Diwani wa kata ya Maganzo ambaye pia ni mwenyekiti wa madiwani wenye kata zinaozunguka mgodi huo alisema anawaomba wananchi waendelee kuwa na utulivu ili baraza huru waliache liweze kufanya kazi yake, kwani hali aliyoiona ni nzuri malalamiko yote yanaenda kushughulikiwa
.






Mkurugenzi mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy akimkabidhi
mwenyekiti wa baraza huru la usuluhishi Dr. Rugemeleza Nshala


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akiendelea kugawa kwa viongozi mbalimbali


Kazi inaendelea ya kugawa vitendea kazi kila sekta inayotakiwa


Mbunge wa jimbo la Kishapu akipokea vitendea kazi kwa ajili ya usuluhishi wa malalamiko ya wananchi waliofanyiwa madhira katika mgodi wa WDL Mwadui

Mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Shinyanga akipokea rasmi vitendea kazi

Mkurugenzi Mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy akimkabidhi rasmi vitendea kazi mkuu wa wilaya ya Kishapu na kuzindua rasmi

Mkurugenzi mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy akimkabidhi vitendea kazi katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese

Diwani wa kata ya Mondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akipokea vitendea kazi za baraza la usuluhishi wa baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi waliofanyiwa madhira

Mkuu w wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzindua rasmi baraza huru
Diwani wa kata ya Maganzo Mbalu Kidiga akizungumza baada ya kuzinduliwa baraza huru la usuluhishi ambapo amewataka wananchi watulie ili baraza hilo lifanye kazi yake

Diwani wa kata ya Idukilo Sara Maiko akizungumza baada ya uzinduzi wabaraza huru la usuluhishi
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru.
Mkurugenzi mkuu wa Petra Diamonds Limited Richard Duffy akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi wa baraza huru.

Mwenyekiti wa baraza huru la usuluhishi Dr. Rugemeleza Nshala akizungumza.

Post a Comment

0 Comments