Header Ads Widget

MGODI WA ALMASI MWADUI WAZINDUA BARAZA HURU KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANANCHI WALIOPATA MADHIRA NDANI YA MGODI HUO

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) akikata utepe kuzindua Baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi ambao wanazunguka Mgodi wa Almasi Mwadui, (kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamond Limited Richard Duffy ambao kwa sasa ndiyo wanafanyashughuli za uchimbaji Almasi ndani ya Mgodi wa Mwadui.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MGODI wa Almasi Mwadui (Wiliamson Diamond), kupitia kampuni ya Petra Diamond, umezindua Rasmi Baraza la huru la kushughulikia Malalamiko ya wananchi ambao wanazunguka mgodi huo na kuyatafutia ufumbuzi ikiwamo kulipwa fidia.

Baraza hilo limezinduliwa leo mkoani Shinyanga na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Mkude akizundua baraza hilo, amesema wananchi ambao wanazunguka Mgodi wa Mwadui, wamepata chombo cha kushughulikia malalamiko yao na kupata haki juu ya madhira ambayo wameyapata katika mgodi huo.

"Baraza hili huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi wanaozunguka Mgodi wa Mwadui, nendeni mkatende haki kwa wananchi na kutatua matatizo ambayo yanawakabili na muwe daraja la kuunganisha mahusiano mazuri," amesema Mkude.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema baraza hilo ndiyo mwisho wa malalamiko ya wananchi juu ya Mgodi wa Mwadui na kutatuliwa matatizo na kuanzisha ukurasa mpya baini ya wananchi na mgodi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Dk. Rugemeleza Nshala, amesema kutokana na kukithiri kwa malalamiko dhidi ya mgodi huo, ndipo likaundwa Baraza huru ambalo litakuwa likishughulikia malalamiko ya wananchi kwa njia ya usuluhishi na kupata haki zao.

Amesema mpaka sasa wana malalamiko 5,575 ya wananchi, ambayo tayari wamesha yasajili na wataanza kuyashughulikia na kutafuta ufumbuzi wake.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamond Richard Duffy, amesema lengo kuu la kuundwa baraza hilo huru, ni kushughulikia malalamiko ya wananchi na kufikia maridhiano na hatimaye kuimarisha mahusiano mazuri baina ya wananchi na mgodi.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamond Richard Duffy, akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi ambao wamepata madhira ndani ya mgodi wa Mwadui ambao kwa sasa wao ndiyo wanaumiliki.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi ambao wamepata madhira ndani ya mgodi wa Mwadui.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi ambao wamepata madhira ndani ya mgodi wa Mwadui

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa baraza hilo.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa baraza hilo.

Post a Comment

0 Comments