Header Ads Widget

HAWA HAPA MAWAZIRI WAPYA WALIOTEULIWA NA WAZIRI MKUU


.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameteua timu yake ya mawaziri katika siku yake ya kwanza.

Katika hotuba yake muhimu nje ya makao makuu ya Waziri mkuu alisema anataka kuleta nchi na chama pamoja, akiahidi utulivu wa kiuchumi na imani.

Mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliona chaguzi zinazoweza kutabirika, na zingine ambazo zimewashangaza wabunge.

Kwa hivyo, tunaweza kusoma nini kuhusu nani anasalia, ni nani anayeenda, na inamaanisha nini?

Kipengele kingine muhimu cha mabadiliko haya ni utulivu katika nafasi tatu za juu: Jeremy Hunt kama kansela, James Cleverly kama katibu wa mambo ya nje na Ben Wallace kama waziri wa ulinzi.

Mojawapo ya teuzi zinazovutia sana ni kurudi kwa Suella Braverman kama katibu wa masuala ya ndani

Alijiuzulu siku chache zilizopita baada ya kukiuka taratibu za usalama, alipotuma hati ya serikali kwa mtu ambaye hajaidhinishwa kuipokea.

Aliidhinisha Bw Sunak kuwa kiongozi mpya siku mbili zilizopita, hatua iliyoonekana kuwa chachu kubwa kwa kampeni yake kwani iliwakilisha uungwaji mkono kutoka kwa mrengo wa kulia wa chama.

Bw Sunak pia amewarudisha wafuasi wengine wakuu kwenye majukumu ya juu - kama Dominic Raab, Steve Barclay na Oliver Dowden. Walikuwa watu muhimu katika kampeni yake wakati wote wa kiangazi, walituzwa kwa uaminifu wao na majukumu serikalini.

Simon Hart pia ameletwa kama kinara mkuu, anayehusika na nidhamu ya chama na ustawi wa wabunge.

Nadhim Zahawi, kansela kwa ufupi majira ya kiangazi, ameshushwa cheo kidogo kutoka kwa waziri wa Ofisi ya Baraza la Mawaziri, kuwa mwenyekiti wa chama - labda kutokana na uungwaji mkono wake wa kutapatapa katika miezi michache iliyopita.

Wakati Bw Sunak amewafikia baadhi ya viongozi wakuu ambao waliwaunga mkono wapinzani wake Boris Johnson na Liz Truss, wengine wameonyeshwa mlango.

Mshirika wa Boris Johnson Jake Berry, mwenyekiti wa zamani wa chama, yuko nje, kama vile Katibu wa zamani wa Usawazishwaji Simon Clarke - msaidizi muhimu wa Liz Truss na mipango yake.

Jacob Rees-Mogg, kama ilivyotarajiwa na wengi, sio katibu wa biashara tena. Siku chache zilizopita, alisema chama kilikuwa nyuma ya Boris - na amemkosoa Bw Sunak waziwazi. Washirika wa Sunak hawatamkosa.

Wawili hawa wamebadilishwa na mwaminifu Grant Shapps kama katibu wa biashara na kurudi kwa Michael Gove kama katibu mkuu, ambaye alishikilia nafasi hiyo chini ya Boris Johnson.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments