Header Ads Widget

WATAALAMU WA AFYA,LISHE NA USTAWI WA JAMII WAPATIWA MAFUNZO ZAIDI JUU YA HUDUMA KWA WATOTO WALIOPATA UTAPIAMLO.
Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji  huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka.

Na  Kareny  Masasy,  Kahama 

WATAALAMU wa afya,lishe na  ustawi wa jamii  kutoka mikoa mitano ya kanda ya ziwa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuwahudumia  watoto  wenye umri chini ya miaka mitano waliopatwa na utapiamlo ili kuondoakana na vifo vitokanavyo na hali hiyo.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 19/09/2022 mjini Kahama  mkoani Shinyanga nakuratibiwa na wizara ya afya ambapo mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Mara na Shinyanga imeshiriki.

 Mwezeshaji wa matibabu ya utapiamlo kitaifa  Getrud  Mollel amesema kuwa jamii inatakiwa iwekeze kwenye umri mdogo wa watoto wao ili kuondokana na taifa tegemezi.

Mollel amesema kuwa wazazi lazima wawajali watoto kwa lishe  bora wenye mpangilio  ili  kuwaepusha na utapiamlo na kuwe na taifa imara  kwa miaka ijayo kwa kuwa na watoto wenye uelewa  mzuri wawapo darasani na kwenye mazingira yanayowazunguka wakuweza kujitegemea bila utegemezi.

Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka ambaye alikuwa mwezeshaji katika mafunzo hayo  amesema hapa nchini   ni asilimia 53 ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano  vimetokea  vikisababishwa na utapiamlo hivyo elimu itolewe kwa wazazi.

Madeleka amewataka maafisa lishe  kanda ya ziwa kutoa takwimu zinazoendana na uhalisia wa maeneo  yao ambapo alieleza kanda ya ziwa bado kuna udumavu kwa watoto ikiwemo mkoa wa Shinyanga una asilimia 32 na Simiyu  ni asilimia 31.

“Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa hali ya lishe uliotolewa na  Tanzania National Nutrition suvey (TNNS) mwaka 2018  umebainisha kuwa ni asilimia 31.8 ya watoto chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa  na asilimia 3.5 wanautapia mlo mkali” amesema Madeleka.

Bundi Clementi ofisa lishe kutoka  halmashauri ya Musoma amesema kuwa wameshukuru kwa kuandaa mafunzo haya kwani wamejifunza kuhudumia watoto wenye utapiamlo mkali  na vitu vya kufanyia kazi kitaalamu.

“Mtoto akiwa na utapiamlo mkali lazima alazwe hata kama hana changamoto zingine za kiafya,akiwa mkodefu lazima uangalie historia alikotokea kwenye jamii nakushirikisha maafisa wa ustawi wa jamii huenda pia  mazingira  anayoishi  ndiyo yamemfanya hivyo" amesema Clement.

Dkt  James Wankuru  kutoka halmashauri ya mji Bunda amesema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwao sababu takwimu zimetolewa nakuelezwa kuwa watoto Millioni tatu wana utapiamlo hapa nchini.

 Dkt Wankuru amesema kuwa   mfumo wa utoaji matibabu kwa watoto wenye utapiamlo umebadilika mojawapo utolewaji wa  matone ya Vitamini A watayatoa kwa wale wenye dalili za utapiamlo na siyo walio nao tayari kama ilivyokuwa zamani.

Wataalamu wakisikiliza mwezeshaji wa mada kwa makini.

Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka
Watlaaamu wa afya,ustawi wa jamii na maafisa lishe kutoka mikoa mitano ya kanda ya ziwa wakipatiwa mafunzo juu ya huduma kwa watoto waliopata utapiamlo na wenye dalili,


Maafisa lishe wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa.
Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka

Mwezeshaji wa wa matibabu ya utapiamlo kitaifa Getrud Mollel.

Mwezeshaji wa wa matibabu ya utapiamlo kitaifa Getrud Mollel.

Post a Comment

0 Comments