` HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI

HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI


HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA IMEPATA HATI SAFI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,imepata Hati Safi kwa hesabu za mwaka wa fedha 2023/2024 unaoishia juni 30.
Hayo yamebainishwa leo Juni 11,2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk.Kalekwa Kasanga,wakati akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),zilizokaguliwa katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2024,kwenye Baraza la Madiwani.

Amesema katika mwaka huo ziliibuliwa hoja 52, hoja mbili zimefungwa,na kubaki hoja 50 ambazo bado utekelezaji wake unaendelea.
“Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kukutaarifu kwamba, kwa hesabu za mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2024, Halmashauri yako imepata Hati Safi,”amesema Dk.Kasanga.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Makana,ameipongeza Halmashauri kwa kupata Hati Safi kutokana kusimamia Rasilimali za Umma vizuri.
Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Mkoa wa Shinyanga CPA Yusuph Mabwe,amesema kwamba utekelezaji wa mapendekezo ya hoja hizo kasi yake iongezeke sababu yanatekelezeka.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwenye Baraza hilo,ameipongeza Halamashuri hiyo kwa kupata Hati Safi,pamoja na kufikisha asilimia 106 ya ukusanyaji wa mapato.
Aidha,ametoa maagizo kwa Hoja 50 ambazo bado utekelezaji wake unaendelea,kwamba ndani ya siku 7 vipatikane vielelezo vya kujibu hoja hizo,na ifikapo tarehe 18 Katibu Tawala wa wilaya,apage kikao katika Halmashauri hiyo wakiwapo na wahusika wote ili zipitiwe hoja baada ya nyingine na vielelezo vyake.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk.Kalekwa Kasanga, akijibu maagizo hayo,amesema atayatekeleza,na kwamba suala la kufungwa kwa Hoja amelipatia kipaumbele na Hoja nyingine zinafungika.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga,akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)kwenye Baraza la Madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akizungumza.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali Mkoa wa Shinyanga CPA Yusuph Mabwe akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464