` JENGO OFISI MPYA YA TAKUKURU KISHAPU LAZINDULIWA

JENGO OFISI MPYA YA TAKUKURU KISHAPU LAZINDULIWA


Na Marco Maduhu,KISHAPU

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Crispin Chalamila,amezindua Rasmi Jengo jipya la Ofisi ya Taasisi hiyo wilayani Kishapu.
Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 25,2025, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali,wananchi na Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo.

Chalamila akizungumza wakati wa uzinduzi huo,amesema Ofisi hiyo mpya itachocheza utendaji kazi kwa ufanisi,pamoja na wananchi kufika kwa wingi kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya Rushwa.
"Shukrani kwa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuiweza Takukuru kwa Rasilimali Watu,Vitendea kazi na ujenzi wa Ofisi,ili kuboresha huduma bora kwa wananchi,"amesema Chalamila.

Amesisitiza kutunzwa kwa Jengo hilo,pamoja na Watumishi wafanye kazi kwa weledi ili kutokomeza Rushwa.

Aidha,ametoa wito kwa shule zote za Msingi na Sekondari kuanzisha Klabu za wapinga Rushwa ili kujenga Taifa la watu Wazalendo.

Amewataka pia wananchi kwamba katika kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu 2025,wasiwachague wagombea watoa Rushwa, wala wasiwaombe Rushwa ili kupata viongozi sahihi watakao waletea maendeleo.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy,amesema Ofisi hiyo mpya wananchi watafika kwa wingi kutoa taarifa za Rushwa, sababu Ofisi ipo katika mazingira Rafiki,tofauti na ilivyokuwa kwenye Jengo la kupanga ambapo walikuwa wakikosa uhuru.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema Takukuru ni Chombo Muhimu kwa maendeleo ya Taifa na kumpongeza Rais Samia kwa ujenzi wa Ofisi za Taasisi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi,amesema wanajivunia kupata Ofisi hiyo mpya,na kutoa wito kwa wananchi walitumie kikamilifu kwa kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya Rushwa.

Naye Mkurugenzi wa Miliki Mhandisi Dk. Emmanuel Kiyabo, akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo hilo, amesema lilianzishwa Januari 27,2024, na kwamba Jumla ya gharama zote hadi kukamilika kwake limetumia sh.milioni 438.3.

Katika hafla hiyo,Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Crispin Chalamila,alisimikwa kuwa Msaidizi wa Machifu Tanzania, na kupewa jina la Mgong'ogong'o.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Crispin Chalamila akizungumza.
Mkurugenzi wa Miliki Mhandisi Emmanuel Kiyabo akizungumza.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akizungumza.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy akizungumza.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Crispian Chalamila akizungumza.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464