Header Ads Widget

TLS-YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA SHERIA NA SERA BILA KUOGOPA


TLS-YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA SHERIA NA SERA BILA KUOGOPA

WAKILI wa mahakama kuu nchini Marry Mwita akitoa mafunzo ya sheria na sera kwa waandishi wanawake walishiriki mafunzo leo septemba 1,2022 jijini Dodoma.







Waandishi wanawake kutoka mikoa mbalimbali Tanzania walioshiriki mafunzo ya sera na sheria kutoka chama cha wanasheria Tanzania(TLS)

Na  Mwandishi wetu.

WAKILI wa mahakama kuu nchini Marry Mwita amewataka waandishi wa habari kutoogopa kuandika habari za kisheria na sera mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha jamii ili wafahamu haki zao.

Wakili Mwita amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wanawake waliokuwa kwenye semina ya siku mbili iliyoanza leo nakufanyika mjini Dodoma kwa kuendeshwa na Tanganyika Law Society (TLS) kwa kusimamiwa na umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC).

Wakili Mwita amesema kuwa upo mchango au nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha sera na sheria zinatekelezwa kwa kushirikisha na wadau wa maendeleo kwani kunatakiwa kundi la watawala na watawaliwa wanaifuata misingi ya sheria iliyo sawa.

"Mwandishi wa habari anapaswa kuzikosoa sera na sheria kandamizi ambazo zimekuwa changamoto ndani ya jamii ni kukazania kuzisoma sio ngumu Kama wanavyozania watumie kalamu zao kuweza kuielimisha jamii pia"amesema Mwita.
Wakili Mwita amesema mwandishi unatakiwa ufanye uchunguzi wa kina katika habari unayotaka kuiripoti ili uweze kumuweka msomaji wako kuamini kwa kuangalia vielelezo na takwimu sahihi.
Ofisa ufuatiliaji na tathimini Selemani Pingoni wa TLS ,amesema kuwa lengo la kuwakutanisha waandishi wa habari wanawake ni kuwaboreshea kwenye kazi zao za kuripoti kwa kutumia kalamu zao na kuangazia maeneo ya taasisi za kidemokrasia na watunga Sheria na sera hizo.

"Sheria Kama ni kandamizi lazima itarudi bungeni kujadiliwa na lazima mwandishi wa habari ujue kazi za bunge, tume ya uchaguzi na tume za haki za binadamu na utawala bora na vyama vya siasa na unavyoripoti mwandishi huegemei upande wowote"amesema Pingoni.

Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo amesema kuwa taasisi ya TLS ni muhimu hapa nchini kwani kila mwandishi anatakiwa kushiriki na kuleta Chachu ya mabadiliko katika eneo lake na yanayofindishwa ni kujua ujuzi na maarifa kwa namna ya kuripoti
Washiriki wakiendelea na shughuli za kujadili kwa makundi juu ya kazi walizopewa na mkufunzi.

WAKILI wa mahakama kuu nchini Marry Mwita akitoa mafunzo.

Post a Comment

0 Comments