Header Ads Widget

ZAHANATI YA KIJIJI CHA NYAMIGEGE YATEKELEZWA KWA MUJIBU WA SERA YA AFYA 2007

 ZAHANATI YA  KIJIJI CHA NYAMIGEGE YATEKELEZWA KWA MUJIBU WA SERA YA AFYA 2007


 Zahanati ya kijiji cha Nyamigege halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekamilika.

 

Na  Kareny  Masasy

SERA ya afya ya mwaka 2007   inaeleza zahanati  kujengwa umbali wa kilometa 5 za mduara na kilometa 10 za mduara kwa kila kituo cha afya, hospitali katika kila wilaya, mkoa na pia hospitali za rufaa na maalum.

Veronika Swela na Shija Manhu wakazi wa kitongoji cha Isanagogo  kijiji cha  Nyamigege kata ya Busangi halmashauri  ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wanasema kuwa  wamefurahi kupata Zahanati karibu wanajua itaanza kufanya kazi  nakupunguza safari ndefu kufuata matibabu.

Swela anasema kuwa  Zahanati imekamilika sasa  wanachosubiri ni  kupata wahudumu  kwani walikuwa wakilazimika kusafiri  kwa  pikipiki  nakutumia gharama  ya sh  10,000 kwenda na kurudi.

 ‘Tulikuwa tunateseka kukosa Zahanati karibu ilibidi tutembee umbali wa  kilomita kumi kwenda Chela kituo cha afya au kilomita  8 kwenda  Zahanati ya kijiji cha Busangi kupata huduma ya kujifungua wakati mwingine ililazimu kujifungua njiani au nyumbani”anasema  Swela.

Mwenyekiti wa kijiji  cha Nyamigege   Anthony Guta anasema kuwa  wananchi wamekuwa wakiteseka kutafuta huduma za afya kwa kukosekana Zahanati karibu  kwani wanatembea umbali mrefu licha ya kuwepo Zahanati kijiji jirani pia hulazimika  kwenda kituo cha afya zaidi ya kilomita kumi kilichopo  kata ya Chela.

“Mwaka 2011 walichanga  wananchi kiasi cha sh Millioni 12 na kuanzisha ujenzi wa jengo la Zahanati  ambalo lilifikia hatua ya kuwekewa paa na  lilikaa muda mrefu bila kukamilishwa na wazazi na wajawazito wanapata shida kupata huduma karibu za kliniki na kujifungua”anasema  Guta.

Diwani wa kata ya hiyo Alexander  Mihayo anasema  kuwa   kijiji hicho  hakina Zahanati na huduma za afya wanazipata  vijiji vya jirani kwa kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano  na wengine kumi  na wajawazito kujifungulia wakati mwingine nyumbani.

“ Kijiji hiki kina vitongoji  vinne  ambavyo ni Kisuke, Isanagogo, Bunangu na Nyamigege  ikiwa Zahanati hii ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2011 nakukamilisha hadi kuezeka paa”anasema  Mihayo .

Mihayo anasema kitu kilichokuwa kimebaki kuweka  ni  saruji sakafuni   na madirisha  na vitu vingine  na hivyo waliachia halmashauri ikamilishe  na pindi ikikamilika wataweza  kuhudumia wakazi 3006 wa kijiji hicho”anasema Mihayo.

Mtendaji wa kata hiyo  Evamary  Elias anasema kuwa  kijiji cha Busangi ndiyo kuna Zahanati  ambayo kijiji cha Nyamigege wakazi wake ndiyo wanakitegemea  lakini kwa kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano wapo wa mama wajawazito  ambao walikuwa wakishindwa kwenda  sababu ya  umbali mrefu nakujifungulia nyumbani.

“Wakazi wa kijiji hiki kila mwaka walikuwa wakitoa kipaumbele chao katika upangaji wa bajeti kuhusu Zahanati ikamilishwe na halmashauri tayari ilitenga bajeti kwa mwaka wa  fedha 2021/22 kiasi  cha shilingi millioni 50 ili kuweza kukamilisha   Zahanati  hii”anasema  Elias.

Mkurugenzi wa Kampuni  ya  Mabao investment  and  general  Pest control Ltd ( AMJ)  Abel Thomas   imetoa  msaada wa  mifuko ya saruji na  giliri   za madirisha   kwa lengo la    ukamilishaji wa  jengo la Zahanati na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya  maeneo ya vijiji  jirani.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abel  Thomas  anasema kuwa kuna  jumla ya mifuko 40  ya saruji na  giri    25 za madirisha nakugharamikia nguvu kazi ya ujenzi  ikiwa vyote kwa pamoja vimegharimu   zaidi ya shilingi Millioni  2.4.

Mganga  mkuu wa  halmashauri  ya Msalala  dkt Ernest  Chacha anasema kuwa kuna vijiji 92  na  tayari vijiji  30 vinazahanati na vituo vya afya vinne   ambazo zinafanya kazi ya kutoa huduma  na  vijiji kumi vimekamilisha Zahanati zinasubiri kupata vifaa tiba na wataalamu kwaajili ya kutoa huduma.

“Kuna fedha ambazo zimekuwa zikitolewa za huduma kwenye jamii  (CSR) na mgodi wa Bulyanhulu  ambazo ilitengwa bajeti yake kwa mwaka wa fedha  2021/22 kiasi cha zaidi ya  shilingi    Billioni  1.245  na  mpaka sasa kimetumika  kiasi cha  zaidi ya  shilingi Millioni 556.8.

Pia dk Chacha anasema   kuwa  mapato ya ndani ya halmashauri  bajeti  ni Billioni 1.5  katika kutekeleza miradi ya afya ikiwemo ujenzi wa Zahanati kupitia fedha hizo” anasema  dk Chacha.

Mbunge wa jimbo la  Msalala  Kassimu Idd anasema kuwa  serikali kuu imeleta fedha   zaidi ya sh Billioni 2  katika sekta ya afya kwaajili ya ujenzi wa majengo ya kutolea huduma mbalimbali pia imeleta wataalamu wa afya 56.


Post a Comment

0 Comments