Header Ads Widget

WANAWAKE KATOLIKI ‘WAWATA’ WAADHIMISHA MIAKA 50 YA UTUME, KABAKA AWAPONGEZA KUWEKA ALAMA UJENZI NYUMBA YA WATAWA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANAWAKE wa Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga, wameadhimisha ya miaka 50 ya utume tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972, na kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuweka alama kujenga nyumba ya Watawa.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Agosti 13, 2022 katika Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akimwakilisha Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Akson.

Akizungumza kwenye Madhimisho hayo,Kabaka  amepongeza kwa kuanzishwa kwa umoja huo wa wanawake wa Katoliki (WAWATA), pamoja na kufanya harambee kwa ajili ya kuacha alama ya kujenga nyumba ya Watawa.

“Mimi hapa leo nimekuwa Mgeni Rasmi nikimwakilisha Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson, na yeye katika harambee hii ameahidi kuweka Sh.milioni mbili kwenye akaunti yenu, na mimi nitatoa Sh.500,000 ili kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Watawa,”amesema Kabaka.

“Kwenye Changizo la leo ahadi ni Sh.milioni Tatu na Fedha taslimu ni Sh.milioni 10.5 hivyo endeleeni kufanya machangizo zaidi ili ujenzi wa nyumba ya Watawa ikamilike na kutimiza adhima yenu ya kuweka alama katika maadhimisho haya ya miaka 50 ya WAWATA,”ameongeza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameahidi kuchangia Sh. 400,000 katika ujenzi wa nyumba hiyo ya Watawa, huku akiwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali ikiwamo kuhamasisha waumini kushiriki kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.

Kwa upande wake Katibu wa Wanawake Katoliki Jimbo la Shinyanga (WAWATA) Beatrice Nangale, amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 1972 na leo imetimiza miaka 50, na malengo yake ni kuwaweka wanawake kuwa pamoja na kutimiza utume wao, ikiwamo kuishi kwa Amani, Upendo, kutafuta haki za wanyonge.

Ametaja malengo mengine ni kupinga vitendo vya ukatili, utoaji mimba, uharibifu wa mazingira, pamoja na kupinga mauaji ya vikongwe, na kubainisha kuwa katika ujenzi huo wa nyumba ya Watawa wamepanga kukusanya kiasi cha Sh.milioni 100.

Kwa upande wake Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu, amesema Wanawake wa Katoliki (WAWATA) kazi yao kubwa ni utume.

Aidha, amewataka kujiamini na kujithamini, kwa kuwa wana mchango mkubwa katika utume wa Kanisa, tangu kuanzishwa kwa chama chao.

Askofu Mkuu Lebulu, ametumia nafasi hiyo kuelezea chimbuko la kuanzishwa kwa utume wa WAWATA miaka 50 iliyopita, na kubanisha kuwa, wamekuwa na mchango mkubwa kupitia karama mbalimbali walizonazo, ikiwemo kuchochea miito ya Upadre na Utawa.

Askofu Mkuu Lebulu, amewataka WAWATA kutambua kuwa, chama hicho siyo chama cha siasa, na badala yake wanapaswa kuzingatia msingi wa kuanzishwa kwake, na kutumia karama walizonazo katika kuujenga ufalme wa Mungu.

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu, akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (UWAWATA) Jimbo la Shinyanga.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga.

Mwenyekiti wa Wanawake wa Katoliki Tanzania Taifa (WAWATA) Evaline Ntenga akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Katibu wa Wanawake Katoliki Jimbo la Shinyanga (WAWATA) Beatrice Nangale, akisoma Risala kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) kwenye maadhimisho hayo. katika Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo.

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea Kanisani.

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea Kanisani.

Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, akishiriki Ibada kwenye Maadhimisho hayo ya miaka 50 ya (WAWATA)

Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, awali, akiwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, (kulia) na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipowasili kwenye Madhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA).

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.

Awali wanawake wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya (WAWATA).

Post a Comment

0 Comments