Header Ads Widget

MCHUNGAJI KKKT SHINYANGA MBARONI TUHUMA KUMLAWITI MTOTO MIAKA 8


MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Makedonia Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga jina (limehifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti Mtoto wa miaka Nane.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuwa tukio hilo limetokea jana


Alisema Jeshi hilo la Polisi lilipata taarifa juu ya Mchungaji huyo, kuwa hua ana mlawiti mtoto huyo wa miaka nane (jina limehifadhiwa) ndipo wakamkamata na wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika hatua nyingine za kisheria zitachukua mkondo wake.

“Jeshi la Polisi hapa Shinyanga tunamshikilia Mchungaji wa Kanisa la KKKT kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka Nane majina yao tumeyahifadhi kwa ajili ya uchunguzi, na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”amesema Magomi.

Post a Comment

0 Comments