Header Ads Widget

NYANI WASABABISHA KIFO CHA MTOTO ALIYEKUWA AKINYONYESHWA NA MAMA YAKE


Mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja amefariki baada ya kuchukuliwa na kundi la Nyani waliotoka kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma wakati akinyonyeshwa na Mama yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama amesema tukio hili limetokea katika Kijiji cha Mwamgongo kilichopo karibu na hifadhi ya Gombe ambapo nyani hao walimnyakua Mtoto huyo mikononi mwa Mama yake aitwae Shayima Kitana aliyekua akimnyonyesha akiwa nyumbani kwake na kutokomea nae porini.

“Kundi hilo baada ya kumvamia Mwanamke huyu lilimtishia na nyani mmoja alimtishia na kuweza kumpora huyo Mtoto mchanga na kuanza kukimbia naye porini, Mama wa Mtoto alipiga kelele kwa kuomba msaada na Wananchi walipofika waliweza kuwafukuza Nyani wale na kumuokoa Mtoto lakini tayari alikua amejeruhiwa kichwani na shingoni na baadaye kwa bahati mbaya akafariki” ——— RPC Manyama.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO millardAyo.

Post a Comment

0 Comments