Header Ads Widget

MWANAFUNZI WA SHULE YA SAMUU AFARIKI KWA KUGONGWA NA BASI LA SHULE YAO

Na Shinyanga Press Club Blog.

 Mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Samuu iliyopo Manispaa ya Shinyanga amefariki baada ya kugongwa na Basi la shule hiyo katika Mtaa wa Majengo mapya Wilaya ya Shinyanga baada ya kumshusha mtoto huyo kisha kumgonga wakati dereva akigeuza basi hilo.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga George Kyando amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni na amemtaja marehemu kuwa ni Godlight Chisawilo mwenye umri wa miaka minne ambaye aligongwa na gari la shule lenye Namba za usajili T. 151 DAG  Toyota Coastar mali ya Malatia wa Shinyanga.

Kamanda amesema basi hilo lilikuwa likitokea shule ya msingi Samuu kuelekea majengo mapya likiendeshwa na dereva  Kassim Said Mahona(40) mkazi wa Nguzonane  Manispaa ya Shinyanga ambaye tayari anashikiliwa na Jeshi la polisi kujibu tuhuma zinazomkabili.

Amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva kutochukuwa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

 

Post a Comment

0 Comments