Header Ads Widget

WATU WANNE WAFARIKI AJALI YA TRENI TABORA

 Mabehewa nane ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora mpaka Dar es salaam yameanguka leo Jumatano Juni 22,2022 katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora na kusababaisha vifo vya watu wanne.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi la polisi linaendelea kufuatilia kutokana na abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.
 

Post a Comment

0 Comments