Header Ads Widget

MBUNGE ATAKA JINA LA HIFADHI YA BURIGI-CHATO LIBADILISHWE

Mbunge ataka jina la hifadhi ya Burigi-Chato libadilishwe

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Ezra Chiwelesa ameiomba serikali kubadilisha jina la Hifadhi ya Burigi-Chato kuwa Burigi ili kusadifu jina la ilipo hifadhi hiyo.

Hifadhi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2019 kwa kuunganisha mapori ya akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi inapatikana katika Wilaya za Biharamulo, Karagwe na Muleba katika Mkoa wa Kagera huku ikiwa umbali wa kilometa 106 kutoka wilayani Chato mkoani Geita.

Amesema umbali huo unaifanya Wilaya ya Chato kukosa sifa ya kuitwa jina la hifadhi hiyo huku akiomba pia geti la kuingilia ndani ya hifadhi hiyo liwekwe katika Wilaya ya Biharamulo ambayo iko karibu na ni umbali wa kilometa 82 kutoka mji wa Biharamulo.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments