Header Ads Widget

MWALIMU MBARONI TUHUMA KUMBAKA MWANAFUNZI DARASA LA SITA

Mwalimu atuhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la sita Njombe

Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia aliyekuwa Mwalimu wa mazoezi (field) Abel Bulugwe (21) kwa tuhuma za kumshawishi na kufanya nae mapenzi Mwanafunzi wake wa darasa la sita (11) mjini Njombe aliyemtorosha kwa usiku mmoja.

RPC wa Njombe Hamis Issa amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia June 4,2022 katika Mtaa wa Indundilanga 
 
“Mwalimu huyu alimaliza field katika Shule hiyo akarudi Chuoni kwake Chuo cha Ualimu Tandala na kumaliza mafunzo ya ualimu na June 01,2022 akarudi Njombe, June 04,2022 alionana nae huyo Binti wakati akienda saloon na Mdogo wake baadaye akaenda nae sehemu alikofikia kwa Rafiki yake”amesema- RPC Issa.

Kwa upande wake Mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo huku akidai kuwa kabla ya kwenda nae nyumbani kwake Binti huyo alimsindikiza nyumbani kwao huku Binti huyo alikataa kuingia nyumbani kwao kwa madai anaogopa kwakuwa amechelewa kurudi “Sikutarajia kama angekuja na kwakweli sikutoa taarifa yeyote, usiku nilifanya naye mapenzi wakati Mtoto mdogo naye alikuwa hapohapo kitandani”- RPC Njombe

Wazazi wa Binti huyo wamesema wamefanikiwa kumpata Mtoto wao mara baada ya kutoa taarifa kwa Wananchi na Viongozi walioanza kutoa ushirikiano huku wakisikitishwa na kitendo cha Mwalimu huyo kwenda kulala na Binti yao huku wakimfanyia ukatili Mtoto wao mdogo kwa kukosa maziwa ya Mama.
soma zaidi hapa Chanzo millardAyo.

Post a Comment

0 Comments