Header Ads Widget

WANAFUNZI WARUHUSIWA KUINGIA NA BUNDUKI DARASANI



Wanafunzi wa vyuo katika jimbo la Texas, Marekani wameruhusiwa kuingia na bunduki darasani.

Hii ni baada ya maprofesa wawili kushindwa kwenye ombi lao la kutaka mahakama izuiwe kutekelezwa kwa sheria mpya inayowaruhusu wanafunzi kubeba bunduki bila kuzionyesha hadharani.


Jaji katika mji wa Austin alipuuzilia mbali madai ya wahadhiri hao kwamba kuwepo kwa bunduki huenda kukawa hatari kubwa iwapo mjadala mkali utazuka darasani.


Mwanasheria mkuu wa Texas, Ken Paxton, ambaye ni wa chama cha Republican, aliunga mkono uamuzi wa jaji.Alisema raia wanaotii sheria wana haki ya kujilinda hata wakiwa kwenye vyuo vikuu.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO BBC SWAHILI.

Post a Comment

0 Comments