Header Ads Widget

SABABU WATUMISHI SITA ARUSHA KUSIMAMISHWA KAZI


Majaliwa awasimamisha kazi vigogo sita Arusha.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi sita wa Halmashuri ya Jiji la Arusha, akiwapo Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk John Pima ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zinazowakabili
Waziri Mkuu amewasimamisha vigogo hao leo Jumanne Mei 24, 2022 baada ya kubaini ubadhirifu unaofanyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwamo kupangisha shule ya msingi binfsi ya mchepuo wa kiingereza ya Sojemu iliyopo Kata ya Muriet.
 
Wengine waliosimamishwa kazi ni Mariamu Mshana ambaye ni mweka hazina wa Jiji hilo, Alex Daniel , Innocent Maduhu na Nuru Kinana kutoka ofisi ya mchumi pamoja na Joel ambao yupo katika Halmashauri ya Longido kwa sasa.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments