Header Ads Widget

SOMA TAARIFA ZA UCHUNGUZI WA AWALI KIFO CHA PADRI ALIYEKUTWA AMEFARIKI NYUMA YA TENKI LA MAJI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kifo cha Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano, Padri Francis Kangwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne Aprili 19, 2022 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro imeeleza kuwa uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zimeonyesha dalili kuwa padre huyo ambaye ni raia wa Zambia anaweza kuwa amejiua.

Padri huyo alikutwa amefariki ndani ya tenki kubwa la maji lililopo nyuma ya nyumba ya makazi ya mapadri Mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman jijini Dar es Salaam.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments