Header Ads Widget

BIBI MBARONI TUHUMA MAUAJI YA MJUKUU WAKE, AMSHUSHIA KIPIGO NA KUMWAGIA MAJI YA MOTO

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanamke Tatu Moshi (45) mkazi wa Lyabukande wilayani Shinyanga, kwa tuhuma za mauaji ya mjukuu wake Joseph Juma (4), baada ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumwagia maji ya moto.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amebainisha hayo leo, wakati akizungumza na vyombo vya habari, kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11 alfajili.

Alisema Bibi huyo amekuwa na tabia ya kupiga wajukuu zake mara kwa mara, kwa madai kuwa wanatabia ya kujisaidia hovyo, na ndipo alipompiga mjukuu huyu sehemu mbaya na kusababisha mauaji, huku mjukuu mwingine Limi Lameck mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba akijeruhiwa vibaya.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tunamshikilia mwanamke Tatu Moshi kwa tuhuma za mauaji ya mjukuu wake, pamoja na mama mzazi wa mtoto huyu Herena Nicolaus, ambaye amekuwa akishuhudia vipigo hivyo na hatoi taarifa juu ya ukatili ambao wanafanyiwa watoto wake na bibi yao,”alisema Kyando.

“Chanzo za mauaji haya ni bibi wa watoto hawa kudai kuwa wajukuu zake wamekuwa na tabia kujinyeanyea hovyo (jisaidia), ndipo akaamua kuwa anawapiga ili waache tabia hiyo, na kusababisha mauaji ya mjukuu wake mmoja baada ya kumpiga vibaya na kumwagia maji ya moto,”aliongeza.

Aidha, Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi na utakapo kamilika bibi huyo atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Post a Comment

0 Comments