Header Ads Widget

SABABU TARURA KUSITISHA FAINI TOZO MAEGESHO YA MAGARI

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), umesitisha kwa muda utozaji wa faini za tozo za maegesho ya magari, baada ya kupokea mapendekezo na maoni ya wadau waliotaka kuongezwa muda wa elimu kuhusu mchakato huo.

Mchakato wa kutoza faini tozo za maegesho kwa njia ya mtandao ulianza rasmi Machi 15, 2022 kwa watumiaji wa maegesho ya Tarura kutakiwa kulipa faini hiyo baada ya kupitisha siku 14.

Lakini baada ya Tarura kuanza kutoza faini hizo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa watumiaji wa maegesho hayo wakidai kutozwa faini kubwa, tofauti na kiwango cha deni linalodaiwa baada ya kupitisha muda wa kulilipa.
 
 SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments