Header Ads Widget

MBARONI KWA TUHUMA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KAMBO



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa Mwaka mmoja na miezi 11.
 
Akizungumza na vyombo vya habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Jana Aprili 8,2022 majira ya saa nane na nusu mchana.

“Tunamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 11”,amesema Kamanda Kyando.

“Mtoto huyo alibakwa na baba yake wa kambo wakati mama wa mtoto huyo akiwa ameenda dukani. Mtuhumiwa amemuoa huyo mama akiwa tayari ana mtoto huyo”,ameongeza Kamanda Kyando.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda unyama huo alimpeleka mtoto huyo kwa mama mwenye nyumba kisha kumwambia kuwa mtoto huyo anatokwa damu kwa sababu amejikata kisu.

Post a Comment

0 Comments