Header Ads Widget

WFT-TRUST YAFANYA MKUTANO KAZI NA MASHIRIKA AMBAYO WAMEYAPATIA RUZUKU YA UTETEZI HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO

Mkurugenzi Mwenza wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania, (WFT- Trust) Rose Marandu akizungumza kwenye mkutano na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo wameyapatia Ruzuku.

Na Marco Maduhu, DAR ES SALAAM

MFUKO wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT Trust), wamefanya mkutano na Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, ambayo wameyapatia Ruzuku ya kutekeleza miradi ya utetezi wa haki za wanawake na watoto, na kuyapatia mafunzo ya utendaji kazi, na namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

Mkutano huo utachukua muda wa siku mbili, ambao umeanza leo Machi 28,2022 jijini Dar es Salaam na utahitimishwa kesho Machi 29,2022.

Mkurugenzi Mwenza wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT Trust) Rose Marandu, akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, amesema lengo kubwa la mkutano huo ni kujifunza, kujengeana uelewa, pamoja na kuunganisha nguvu ya pamoja (TAPO) katika kumkomboa kimapinduzi mwanamke na mtoto wa kike, na kupata fursa sawa katika nyanja mbalimbali zikiwemo za elimu, kiuchumi, na uongozi.

Alisema Mfuko huo wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania, (WFT Trust) wameamua kufanya mkutano kazi na Mashirika ambayo wameyapatia Ruzuku ya utekelezaji wa miradi ya utetezi wa wanawake na watoto, ili kuendelea kujengeana uelewa, uzoefu, kubadilisha mawazo, na kujifunza namna ya mchakato wa kupata Ruzuku.

“Mkutano wetu huu ni muhimu sana, ambao utadumu ndani ya siku mbili na utakuwa na mambo mengi ya kujifunza, na mkutano hautakuwa kama darasa, bali utakuwa wa kujifunza na kujengeana uwezo zaidi juu ya mfuko wetu wa utoaji wa Ruzuku,” alisema Marandu.

“Katika Mkutano huu pia mtapata uelewa mpana wa juu ya mfuko wetu wa utoaji wa Ruzuku, (WFT Trust) ili kuendana na mpango mkakati wetu wa Nne ambao tumeutengeneza, ulioanza (2021-2025) ili muelewe tunakwenda wapi na tunataka kufanya vitu gani, na mtapata kwa ufupi utaratibu wetu wa utoaji wa Ruzuku,” aliongeza.

Aidha, alisema wao kama Women Fund Tanzania Trust, huwa wanatoa Ruzuku kwenye mashirika, ili kuongeza sauti katika utetezi wa haki za wanawake na watoto, na kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia ndani ya jamii, pamoja na kupinga Mila na Desturi kandamizi zinazo mkandamiza Mwanamke na Mtoto wa kike na kukosa haki zao.

Pia, alitaja njia tatu za ujenzi wa nguvu ya pamoja (TAPO) kwa ajili ya kupinga masuala ya mfumo dume ili kuleta ukombozi wa mwanamke kimapinduzi, kuwa ni kuwapa fursa wanawake kwenye nafasi za uongozi, kupinga Rushwa ya Ngono, na kuwapa haki ya Afya ya Uzazi hasa katika likizo ya uzazi na unyonyeshaji watoto.

Kwenye mkutano huo zilitolewa mada mbalimbali za kuwajengea uwezo mashirika hayo, ikiwemo ya ujenzi wa Tapo kimapinduzi, Masuala ya Fedha, kuandika maandiko ya mradi, namna ya kuomba Ruzuku, tathimini na ufuatiliaji wa miradi, na jinsi ya kuwasilisha matokeo.

Mkurugenzi Mwenza wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania, (WFT- Trust) Rose Marandu akizungumza kwenye mkutano na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo huyapatia Ruzuku.

Carol Mango akiwasilisha Mada namna ya kuandika maandiko ya mradi kwenye mkutano huo.

Brian Mshana akiwasilisha Mada maombi ya Ruzuku kwenye mkutano huo.

Dorice Tesha, akiwasilisha Mada ya ujenzi wa TAPO kimapinduzi.

Stella Kihiyo, akiwasilisha Mada namna ya kuandaa Ripoti za Fedha kupitia Ruzuku ambazo huwapa Mashirika hayo.


 
Redimna Ginwas akiwasilisha Mada ya Tathimini na ufuatiliaji wa Miradi.
,
Wilma Mallya akiwasilisha Mada ya jinsi ya kuwasilisha Matokeo ya utekelezaji wa Miradi.

Washiriki kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakiwa kwenye Mkutano wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust).

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Washiriki wakiendelea na Mkutano.

Kwa mawasiliano zaidi kwa WFT Trust, Piga simu +255 753 912 130, tuma barua pepe kwa info@wftrust.or.tz au tembelea tovuti www.wft.or.tz.

Post a Comment

0 Comments