Header Ads Widget

AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU

 Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia Mohamedi Lukindo (43) mkazi wa Chanika wilayani Handeni akituhumiwa kumshambulia hadi kufa Athumani Dolly (46) akidai kumfumania na mkewe nyumbani kwake usiku.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu Athumani, ameuawa usiku wa kuamkia Jumatatu Machi 28 baada ya kukutwa ndani na mume wa Rehema Barau majira ya usiku na kuanza kumshambulia.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa wa mauaji kumshambulia hadi kufa kijana aliyemkuta ndani kwake na mkewe ambapo polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua undani wake, muhusika aliyefanya tukio hilo ameshakamatwa.

 SOMA ZAIDI HAPA; CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments