Header Ads Widget

WATOTO UMOJA WA MAKANISA YA CCT SHINYANGA WAFANYA MAOMBI YA DUNIA YA WATOTO, WATAKA AMANI NCHI ZA UKRAINE NA URUSI


Watoto kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye maombi ya watoto duniani, katika Kanisa la Anglikana Lubaga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WATOTO kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wamefanya maombi ya dunia ya watoto, huku wakiwakumbuka kweye maombi watoto wenzao, ambao wapo kwenye nchi za Ukraine na Urusi ambazo zinazoendelea kupigana vita.

Maombi hayo yamefanyika Marchi 12, 2022 katika Kanisa la Aglikana Lubaga Manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kanisa la AIC Kambarage, Kitangili, Ngokolo, Moraviani, Menonite, KKKT Makedonia, Ebenezer, Azimio, Kitangili, Busongo, Ndala, Angaza, na Bushushu Chaplaincy.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto kutoka Kanisa la KKKT Makedonia Holiness Harold, akisoma Risala kwa niaba ya watoto wote wa umoja huo wa Makanisa ya kikristo, kwa Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa Nacy Kasembo, ambaye alihudhulia maombi hayo ya watoto dunia Kanisani hapo.

Alisema watoto hawapendezwi na mapingano ya vita ambayo yanaendelea katika nchi mbili za Ukraine na Urusi kuwa miongoni mwa waathirika wa vita hiyo ni watoto, ambapo katika maombi yao wamewakumbuka na kuwaombea, pamoja na vita hiyo imaridhike katika nchi hizo na amani itawale, ili watoto waendelee na masomo yao na kutimiza ndoto zao.

“Katika maombi yetu ya kila siku, tuendelee kuwaombea watoto wenzetu ambao wapo katika nchi zinazopigana vita Ukraine na Urusi ili wabaki kuwa salama, pamoja na vita imalizike na kurudi katika hali ya kawaida ya amani,”alisema Harold.

Pia waliiomba jamii iendelee kushikamana pamoja na kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo, huku akibainisha matamanio ya watoto wa Shinyanga ni kuongoza kitaaluma, na siyo kwa vitendo vya ukatili dhidi yao.

Katika hatua nyingine waliipongeza Serikali kwa kuunda mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya kijiji, ambayo yatakuwa msaada kwao kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao na kuendelea kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao, na kuwaomba wazazi waendelee kuruhusu watoto wao wajiunge kwenye mabaraza hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa Nancy Kasembo, alikazia suala la watoto kuendelea kuombea watoto wenzao ambao wapo katika nchi hizo zinazopigana vita Ukraine na Urusi, pamoja na amani itawale ili waishi katika maisha yao ya kawaida,

Aliwataka pia watoto wote hapa nchini wawe wanatoa taarifa za matukio ya ukatili, ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria na kukomesha vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto kutoka Kanisa la KKKT Makedonia Holiness Harold, akisoma Risala kwa niaba ya watoto wote wa umoja huo wa Makanisa ya kikristo, kwenye maombi hayo ya watoto duniani.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa Nancy Kasembo, akizungumza kwenye maombi hayo ya watoto dunia, ambayo yamefanyika katika Kanisa la Anglikana Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Watoto kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye maombi ya watoto duniani, katika Kanisa la Anglikana Lubaga.

Watoto kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye maombi ya watoto duniani, katika Kanisa la Anglikana Lubaga.

Watoto kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye maombi ya watoto duniani, katika Kanisa la Anglikana Lubaga.

Watoto kutoka umoja wa Makanisa ya kikristo Tanzania (CCT) Manispaa ya Shinyanga, wakiingia na maandamano kwenye maombi hayo ya watoto duniani katika Kanisa la Anglikana Lubaga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments