Header Ads Widget

SIMBA YAENDELEZA USEMI KWA MKAPA HATOKI MTU, YAICHAPA RBS BERKANE BAO 1-0

 WAWAKILISHI Pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Simba SC wameendelea kuwa tishio katika uwanja wa Benjamin Mkapa  baada ya kuichapa bao 1-0 RSB Berkane ya Morocco katika  Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa  jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Simba ni winga hatari Papa Sakho aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 44 baada ya kuichachafya ngome ya Berkane na kupiga shuti ndani ya kumi na nane na kumuacha Mlinda mlango hana la kufanya.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko pamoja kushambuliana kwa zamu huku Simba wakikosa nafasi nyingi za kufunga.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 7 na kuchupa hadi nafasi ya kwanza katika kundi D huku Berkane wakishuka nafasi ya pili wakiwa na Pointi 6,Nafasi ya tatu US Gendarmerie Pointi 4 na ASEC Mimosas wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na Pointi 3.

Mchezo mwingine wa Kundi hilo utachezwa majira ya saa moja usiku ASEC Mimosas watakuwa nyumbani kucheza na US Gendarmerie

Post a Comment

0 Comments