Header Ads Widget

WASHITAKIWA 12 KESI ZA UGAIDI WAACHIWA HURU KISUTU


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta kesi tano za ugaidi na kuwaachia huru kwa masharti washtakiwa 12, waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kujihusisha na vitendo vya ugaidi.

Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Washtakiwa hao Seif Mwishehe, Yusuph Rajabu, Buheti Buheti, Juma Athuman, Ally Nassoro maarufu kama Omary Swala, Hassan Mnele na wenzao sita.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hizo umetolewa leo Jumanne Machi Mosi, 2022 na Mahakimu watano tofauti, ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi, Huruma Shahidi na Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Post a Comment

0 Comments