Header Ads Widget

WANAFUNZI WAAFRIKA WADAI KUBAGULIWA UKRAINE


Wanafunzi Waafrika wanaosoma nchini Ukraine wamedai kuwa wanabaguliwa na vikosi vya usalama wanapokuwa katika harakati za kuikimbia nchi hiyo kuelekea nchini Poland.

Mmoja wa wanafunzi hao wa Afrika aliyezungumza na shirika la habari la CNN, amesema yeye na wenzake walitakiwa kushuka katika usafiri wa umma katika kituo cha ukaguzi katika mpaka wa Ukraine na Poland.

Mwanafunzi huyo amesema waliambiwa wakae pembeni wakati basi linaondoka na raia wa Ukraine pekee yao.

“Zaidi ya mabasi 10 yalikuja na tulikuwa tukiangalia wakati wengine wakiondoka. Tulifikiria baada ya kuwachukua raia wa Ukraine watatupeleka sisi, lakini walituambia hapakuwa na mabasi mengi tena na tuliambiwa tutembee,” amesema.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.
 

Post a Comment

0 Comments