Header Ads Widget

MWANAMKE ALIVYOMSAIDIA MUMEWE KUMBAKA MWANAWE WA MIAKA MINNE


Si rahisi kuamini lakini ilitokea huko Mbarali, mkoani Mbeya bila kuripotiwa.

Hiki ni kisa cha kusikitisha cha mtoto wa miaka minne, *Jane Mwikila (si jina halisi), aliyebakwa na baba yake wa kambo na kuharibiwa sehemu za siri huku mama yake mzazi akisaidia kutekelezwa kwa unyama huo. 
Elias Mwangoka, maarufu kwa jina la Kingloli, alifanya ukatili huo asubuhi ya Aprili 30, 2006 katika Kijiji cha Muhelwa, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya huku mke wake, Agnes Mwakisyala akimsaidia kwa kumbana miguu mwanawe asifurukute.
 
Baada ya kukwepa mkono wa dola kwa miaka minne, hatimaye Mwangoka alikamatwa mwaka 2010, akashtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Atasalia huko kwa maisha yake yaliyobaki baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa yake ya hivi karibu aliyokuwa akipinga adhabu aliyopewa... ENDELEA KUSOMA HAPA CHINI KWA KUBONYEZA HIYO LINK PALIPO ANDIKA SOMA HAPA👇
 
SOMA HAPA ZAIDI ;CHANZO MWANANCHI.
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807