Header Ads Widget

WANAFUNZI 84 WAPEWA UJAUZITO SHINYANGA, RC MJEMA AAGIZA KESI ZOTE ZA MIMBA ZIFUATILIWE NA KUCHUKULIWA HATUA


Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, akiwasilisha taarifa ya elimu kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa na kutoa takwimu za wanafunzi waliopewa ujauzito na kukatisha masomo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANAFUNZI 84 wa shule za msingi na Sekondari mkoani Shinyanga, wameripotiwa kupewa ujauzito mwaka jana na kukatisha masomo yao.

Hayo yamebainishwa leo March 3, 2022 na Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoani Shinyanga, kilichokuwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha elimu mkoani humo.

Alisema baadhi ya changamoto ambazo wanakumbana nazo kwenye Sekta ya elimu mkoani Shinyanga ni baadhi ya wanafunzi kushindwa kumaliza masomo yao ya elimu ya msingi na kidato cha Nne, kuwa inatokana na utoro pamoja na wanafunzi wa kike kupewa ujauzito.

Ametaja takwimu za wanafunzi ambao wamehitimu elimu ya msingi mwaka jana , kuwa waliandikishwa kuanza darasa kwanza wakiwa 48,298 lakini waliohitimu ni 38,694 huku wanafunzi 9,604 hawa kuhitimu elimu hiyo ya msingi kutokana na utoro pamoja na mimba za utotoni.

Pia ametaja takwimu za wanafunzi wa shule ya Sekondari ambao wamefanikiwa kuhitimu kidato cha Nne kuwa ni 13,989, ambapo waliandishwa wanafunzi 19,213, huku 5,224 alishindwa kuhitimu elimu hiyo.

“Changamoto ambazo zinatukabili wanafunzi kushindwa kumaliza masomo yao ni utoro pamoja na mimba za utotoni, mfano kwa takwimu za mwaka jana wanafunzi 27 wa shule za msingi walipewa ujauzito, na wanafunzi 57 kutoka Sekondari,” alisema Ndalichako.

“Kesi za mimba hizi zipo mahakamani, nyingine kwenye upelelezi na baadhi zimeshatolewa hukumu,”aliongeza.

Aidha, alisema kwa upande wa utoro inasababishwa na ukosefu wa ulaji wa chakula shuleni ambapo baadhi ya wanafunzi wanasoma umbali mrefu hasa wale ambao wanasoma katika shule za Kata, ambapo njaa inapowazidi hutoroka shule na wengine kuamua kuacha kwenda kabisa.

Katika hatua nyingine alisema mkoa huo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu, hali ambayo inasababisha wanafunzi kushindwa kufundishwa kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, aliagiza kesi zote za mimba zifuatiliwe pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, akizungumzia upande wa chakula amewaagiza Wakuu wa wilaya, na viongozi ngazi ya Halmashauri kuweka mikakati ya kuanza utoaji wa chakula mashuleni kwa kushirikiana na bodi na kamati za shule, ili wanafunzi wapate chakula na kuacha utoro na kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Amesema kwa shule za msingi ambazo zinatoa chakula mkoani humo ni asilimia 22, ambapo kwa Sekondari ni asilimia 46, na kubainisha kuwa mtoto akisoma akiwa na njaa kamwe hawezi kuelewa masomo vizuri.

Pia ameonya tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipotosha kuwa elimu kwa sasa ni malipo, na kuwataka wananchi wapuuze taarifa hizo ambapo elimu inatolewa bure, huku akiwasisitiza waendelee kupeleka watoto wao kaundikishwa shuleni, ili baadae waje kuwasaidia na tegemeo kwa taifa.

Amesema kwa Takwimu hadi sasa za wanafunzi ambao wameandikishwa darasa la awali ni aslimia 88, kwanza asilimia 97, huku kidato cha kwanza asilimia 83, ambapo bado uandikishaji wanafunzi unaendelea hadi Marchi 31 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mjema, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi la uandikishaji sense na makazi ambalo litafanyika Agost Mwaka huu, pamoja na kuendelea kujikinga na janga la maambukzi ya virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga.

Katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoani humo.

Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, akiwasilisha taarifa ya elimu kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoani humo.

Viongozi wakiwa kwenye kikao cha elimu.

Viongozi wakiwa kwenye kikao cha elimu.

Viongozi wakiwa kwenye kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.

wajumbe wakiendelea na kikao cha elimu.
 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments