Header Ads Widget

AJIUA BAADA YA KUUWA MKE NA MTOTO KWA KUWAKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Joseph Paul, akitoa taarifa ya tukio la mauaji kwa vyombo vya habari

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Madirisha Kanyalu (60) mkazi wa kitongoji cha Mwamadulu kijiji cha Bulambila Kata ya Mwalukwa wilayani Shinyanga, amefariki dunia kujitumbukiza kwenye dimbwi maji, mara baada ya kumuua mkewake Evodia Nyerere (27), na Mtoto wake Meshack Madirisha mwenye umri wa miezi 11, kwa kuwakata na kitu chenye ncha kali shingoni.
 
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Joseph Paul, akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana, alisema tukio hilo limetokea Marchi 2 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi ndani ya nyumba yao.

Alisema mwanaume huyo ambaye ni marehemu, mara baada ya kumaliza kuuwa familia yake, alikwenda kujitumbukiza kwenye dimbwi la maji lililokaribu na nyumba yake aliyokuwa akiishi na kufariki dunia.

“Chanzo cha tukio hili ni Mgogoro wa kifamilia, ambapo mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na wanaume wengine,”alisema Paul.

Aidha, alisema miili ya marehemu hao wote watatu walipelekwa kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga, na kuabinisha kuwa kwasasa wamesha kabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda, alitoa wito kwa wanandoa mkoani humo wawe wanapeleka malalamiko yao mapema kwenye dawati la jinsia la Jeshi hilo, pamoja na ustawi wa jamii ili kupata suluhisho la migogoro yao, kuliko kujichukulia sheria mkononi na kusababisha mauaji.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments