Header Ads Widget

SABABU MAKAHABA WANAUME NA WAKE ZA WATU WANAVYO ONGEZEKA KUFANYA BIASHARA YA KUUZA NGONO


Mamlaka nchini Iran imekuwa ikisema kuwa hakuna ukahaba nchini humo

"Ninaona aibu kwa kile ninachofanya, lakini nina chaguo gani?" anasema Neda, mtalaka wa huko Tehran.

Wakati wa mchana amekuwa akifanya kazi kama msusi wa nywele, lakini usiku anafanya kazi yake ya pili kama kahaba, akihisi kulazimishwa kuingia kwenye biashara hiyo ya kuuza mwili wake kwa ngono ili kupata mkate wake wa kila siku.

"Ninaishi katika nchi ambayo wanawake hawaheshimiwi, uchumi unayumba, na bei ya kila kitu inapanda karibu kila siku," anasema. "Nalea mtoto mwenywe bila baba. lazima nimtunze mwanangu. Ukahaba hulipa vizuri, na sasa ninapanga kununua nyumba ndogo jijini. Huu ndio ukweli wa kusikitisha wa maisha yangu. kwa kweli ninauza utu wangu."

Mwaka 2012, Iran ilitangaza mpango wa kitaifa wa kukabiliana na ukahaba. Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na watafiti, idadi ya watu wanaofanya kazi katika sekta hiyo ya ukahaba imeongezeka.

Nchi hiyo ya kidini ya kihafidhina ya Iran kwa muda mrefu imekuwa ikikanusha kuwepo kwa wauza ngono au makahaba nchini humo. Badala yake, mamlaka zinaelezea ukahaba huko kama njama ya Magharibi iliyoundwa kuwapotosha vijana, au kuwatupia mzigo wa lawama wanawake kwa kuwapotosha wanaume wasio na maadili.

Takwimu zisizo rasmi pia zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa ngono wa Iran wanapungua. Takwimu kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali zinaonyesha kuwa mwaka 2016 wasichana wenye umri wa miaka 12 walijihusisha na ukahaba.

Shirika la Aftab Society, shirika lisilo la kiserikali lililojitolea kuwasaidia wanawake wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini Iran, lilisema mwaka 2019 kwamba kunaweza kuwa na makahaba 10,000 katika mji mkuu, takribani asilimia 35% kati yao ni wake za watu.


SOMA HAPA ZAIDI CHANZO BBC SWAHILI.

Post a Comment

0 Comments