Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUENDELEZA MEMA YA HAYATI JOHN MAGUFULIRais Samia Suluhu Hassan amesema mema yote yaliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli yataendelezwa

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 17, 2022 alipokuwa akitoa salamu za taifa katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa kumbukizi ya kifo cha hayati Magufuli.

Rais Samia ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na nidhamu, uadilifu na kupiga vita ubadhilifu.

"Hivi karibuni tutafungua daraja la Tanzanite lililoko jijini Dar es salaam hii ilikua ndoto ya Magufuli na nitaiendeleza kwa kuboresha huduma za maji, umeme na miundombinu"amesema Samia

Akizungumzia miradi iliyopo Geita, Rais Samia amesema mradi wa kivuko cha Chato-Nkome kilichogharimu Sh3.1 bilioni umekamilika.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANACHI.

Post a Comment

0 Comments