Header Ads Widget

MATUKIO YA MAUAJI DODOMA YATIKISA, POLISI WANYOOSHEWA KIDOLE


Picha aihusiani na matukio ya mauaji Dodoma

Matukio ya mauaji katika mkoa wa Dodoma yanatajwa kuongezeka katika siku za hivi karibuni, huku sababu za mauaji hayo zikitofautiana na baadhi ya watu wakilinyooshea kidole Jeshi la Polisi kuwa linashindwa kutimiza wajibu wake.
Mbali na mauaji hayo, visa vya watu kujeruhiwa kwa mapanga na nondo vinatajwa kuongezeka katika mitaa ya katikati jijini Dodoma licha ya Polisi kukiri kuwakamata waharifu wengi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga, alikiri kuwapo kwa matukio hayo ambayo yanahusisha pia wizi wa magari, pikipiki na kukamatwa kwa nyara za Serikali na dawa za kulevya. Mpaka sasa watu watu 67 wanashikiliwa.

Kati ya Februari 25,2022 hadi Machi 11, 2022 kulitokea mauaji ya watu wawili kwenye maeneo tofauti, moja likihusisha mwanamke aliyekatwa mapanga asubuhi akienda kazini Mtaa wa Mtumba na mvulana mwenye umri wa 22)ambaye aliuawa katika ugomvi wa kugombea Sh400 ambayo ilikuwa chenji ya sigara.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments