Header Ads Widget

SABABU ASKOFU MWAIKALI KUMPINGA ASKOFU SHOO UCHAGUZI DAYOSISI YA KONDE

Siku moja baada ya kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo kumtangaza Geofrey Mwakihaba kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Konde, Askofu Dk Edward Mwaikali amesema hatambui mabadiliko hayo kwa sababu hajajulishwa chochote.
 
Kwa muda mrefu kumekuwapo na mgogoro katika Dayosisi hiyo hali ambayo imekuwa ikihatarisha amani kwa waumini wa dhehebu hilo hasa baada ya kuhamishwa kwa makao makuu kutoka Tukuyu kwenda Mbeya mjini.

Katika mkutano uliofanyika jana Jumanne Machi 22, 2022 jijini Mbeya ulifanyika uchaguzi kufuatia tume iliyoundwa na Dk Shoo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Dk Mwaikali ambaye ni Askofu Mkuu wa kanisa hilo.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments