Header Ads Widget

KONGAMANO LA WANAWAKE MKOANI SHINYANGA LAFANA, RC MJEMA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake mkoani humo.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

KONGAMANO la wanawake mkoani Shinyanga, ambalo limeendana na uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, limefana mkoani humo, ambalo limekutanisha wanawake wa mkoa huo kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na upataji wa haki zao.

Kongamano hilo limefanyika leo March 6,2022 wilayani Kahama, kwa kukutanisha wanawake wote wa Mkoa wa Shinyanga, ambalo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani March 8.

Mjema akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, amesema wanawake ni kundi kubwa katika kuleta maendeleo ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo kupitia jukwaa hilo watajadili fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zipo mkoani Shinyanga, pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.

Alisema Mkoa wa Shinyanga una fursa nyingi za kiuchumi zikiwamo za madini na kilimo, lakini fursa hizo kwa upande wa wanawake kiuchumi zimekuwa zikiwekwa pembeni na kunyimwa haki zao.

"Kupitia Kongamano hili la wanawake, natarajia mpate mtandao wa kufanya biashara na kukua kiuchumi, na baada ya miaka 10 nataka niache alama hapa mkoani Shinyanga kuwepo na idadi kubwa ya wanawake ambao ni matajiri na wenye kumilika mali mbalimbali," alisema Mjema.

"Nawapongeza pia wanawake wa mkoa wa Shinyanga kwa kujituma kufanya shughuli mbalimbali, ambapo tangu nifike hapa Shinyanga nimeona wanawake wengi wakijishughulisha, hivyo natoa wito kwa wanawake msikae bila kufanya kazi fursa zipo nyingi zitumie kujikwamua kiuchumi," aliongeza.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Wakuu wa wilaya wote mkoani humo, kuweka mikakati ya kuandaa makongamano ya wanawake kila baada ya miezi mitatu, ili waendelee kujadili mambo mbalimbali, zikiwamo fursa za kiuchumi na kupata haki zao.

Pia amewataka wanawake mkoani humo, kuendelea kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani katika masuala ya kimaendeleo na kiuchumi, kama kauli mbiu ya Kongamano hilo inavyosema "Amka mwanamke kazi iendelee".

Katika hatua nyingine Mjema amewataka wanawake mkoani Shinyanga, kuvunja ukimya juu ya vitendo ya ukatili wa kijinsia ambavyo wamekuwa wakifanyiwa, na kuacha kukaa na maumivu hayo na hata kuwasababishia ulemavu na vifo, bali wapaze sauti kufichua vitendo hivyo na kuishi salama.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, alisema malengo mahususi ya Kongamano hilo la wanawake, ni kufahamiana, kubadilishana mawazo pamoja na kujenga mtandao wa kibiashara na kuinuana kiuchumi.

Alisema malengo mengine ni kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zipo ndani ya mkoa wa Shinyanga, ili kuzitumia na kupata maendeleo.

Nao baadhi ya wanawake wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga, kwa kuandaa Kongamano hilo, ambalo limewafumbua na kubadilisha uzoefu wa kibiashara na kuinuka kiuchumi.

Kongamano hilo la wanawake mkoani Shinyanga, lilihudhuliwa pia na Wabunge wa Vitimaalum mkoani humo, akiwamo Santiel Kirumba, Ruth Mayenga, Mwenyekiti wa UWT Magret Cosmas, Hakimu Mfawidhi wa Mkoa Mary Urio, Mwakilishi wa mfuko wa Ruzuku wanawake Tanzania (WFT) Glory Mbia.

Kwenye Kongamano hilo zilotolewa pia Mada mbalimbali, zikiwamo za uchumi, ukatili wa kijinsia, na utolewaji wa shuhuda kwa wanawake ambao walitumia fursa za kiuchumi za Mkoa huo wa Shinyanga na kufanikiwa kimaisha.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake mkoani humo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake CCM (UWT)Mkoa wa Shinyanga Magreth Cosmas akizungumza kwenye Kongamano hilo la Wanawake.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akizungumza kwneye Kongamano hilo la Wanawake.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Ruth Mayenga akizungumza kwneye Kongamano hilo la Wanawake.

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoani Shinyanga Rehema Edson, akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoani Shinyanga Regina Malima, akizungumza kwenye Kongamano hilo la Wanawake.

Utoaji wa mada ukiendelea kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Utoaji wa mada ukiendelea kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Viongozi mbalimbali wanawake mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano lao.

Viongozi wanawake mkoani Shinyanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (watatu kutoka kushoto) wakipiga picha ya pamoja kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Viongozi wanawake mkoani Shinyanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (watatu kutoka kulia) wakipiga picha ya pamoja kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo la Wanawake mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo la Wanawake mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo la Wanawake mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo la Wanawake mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo la Wanawake mkoani Shinyanga.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwasili kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Na Marco Maduhu, KAHAMA.

Post a Comment

0 Comments